Afisa Utumishi wa kampuni ya teknolojia na mawasiliano Vodacom Tanzania Plc Gervas Mfubusa akikabidhi zawadi kwa mwakilishi wa kikundi cha TEF’s Orphanage Center Farida Maside baada ya kikundi chao kuibuka kuwa na nidhamu bora wakati wa mafunzo ya TEHAMA yaliyopewa jina la ‘Code like a girl’, mpango unaoendeshwa na Vodacom Tanzania kupitia Taasisi isiyo ya Kiserikali ya dLab ili kuhamasisha wasichana kupenda masomo ya Sayansi. Mafunzo hayo yamefanyika jijini Dar es Salaam.
Afisa Utumishi kwa kampuni ya teknolojia na mawasiliano Vodacom Tanzania Plc Gervas Mfubusa akitoa zawadi kwa mwakilishi wa kikundi cha Tanzania Safari Adventures Keziah Mafuru baada ya kushinda nafasi ya kwanza kwenye mafunzo ya TEHAMA yaliyopewa jina la ‘Code like a girl’, mpango unaoendeshwa na kampuni hiyo kupitia taasisi ya dLab ili kuhamasisha wasichana kupenda masomo ya Sayansi. Mafunzo hayo yamefanyika jijini Dar es Salaam.
Afisa Rasilmali Watu wa kampuni ya teknolojia na mawasiliano Vodacom Tanzania Plc Gervas Mfubusa akiongea na washiriki wa mafunzo ya TEHAMA yaliyopewa jina la ‘Code like a girl’, mpango unaoendeshwa na Vodacom Tanzania kupitia Taasisi isiyo ya Kiserikali ya dLab ili kuhamasisha wasichana kupenda masomo ya Sayansi. Mafunzo hayo yamefanyika jijini Dar es Salaam.
0 Comments