Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe.Abdallah Ulega akizungumza na wafugaji na wenye viwanda vya kuchakata nyama hapo jana Jijini Dar es Salaam (Picha na Emmanuel Mbatilo)
****************************
NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe.Abdallah Ulega ameielekeza Bodi ya Nyama nchini kutengeneza mfumo mzuri wa kuhakikisha biashara ya unenepeshaji mifugo inashamiri kwani ni fursa kubwa kwa wafugaji wa asili kuingia kwenye fursa hiyo.
Ameyasema hayo jana Jijini Dar es Salaam katika kikao alichokaa na wafugaji na wenye viwanda vya kuchakata nyama na kujadili ni namna gani wanaweza kutumia fursa zilizopo ili kuweza kunufaika na mifugo iliyopo nchini.
Akizungumzia katika kikao hicho, Mhe.Ulega amesema kuingia kwa wafugaji wa asili katika biashara ya kunenepesha mifugo inawezekana ng'ombe zao zisikubali kwa urahisi kunenepa lakini hivyohivyo kwani kila jambo lazima lianze, elimu ipelekwe ya kutosha ya unenepeshaji wa mifugo.
Amesema viwanda vilivyopo mpaka sasa vinahitaji mifugo pia na sifa zinazopatikana kwenye soko hivyo wafugaji wametakiwa kuchangamkia fursa.
"Soko linafunguka zaidi, tumeona Mheshimiwa Rais amekaribisha masoko makubwa duniani ikiwemo soko la Saudi Arabia lakini kupitia masoko haya tunatakiwa tuungane sote kujua soko linataka nini na fursa ni kubwa". Amesema Mhe.Ulega.
0 Comments