NA TIGANYA VINCENT
MKUU wa Mkoa wa Tabora Balozi Dkt.Batilda Buriani ameagiza Uongozi wa Halmashauri ya Manispaa ya Tabora kuanzisha operesheni ya kusafisha maeneo kwa kuwamata watu wote wanaotupa takataka mitaani.
Alisema hali ya usafi katika maeneo mengi ya Manispaa ya Tabora haurishidhi na kuwataka kutumia Sheria zilizopo kuwaadhibu wanachafua mji kwa kutupa takataka kwenye maeneo mbalimbali ikiwemo kwenye mitaro ya barabara.
Balozi Dkt. Batilda alitoa kauli hiyo jana mjini hapa wakati wa uzinduzi wa Baraza la Biashara la Manispaa ya Tabora.
Alisema kuwa Sheria ya Mazingira, Sheria ya Mistu na Sheria ndogo ndogo za Manispaa hiyo zitumike kuwatoza faini watakaokamatwa wakitupa taka na kuharibu mazingira ili kutoa fuzo kwa wengine.
Balozi Dkt. Batilda alisema ni lazima wananchi wafundishwe kupenda usafi kama njia mojawapo ya kuupendezesha mji na kujikinga na magonjwa ya mlipuko.
Alisema kama wakazi wa Mikoa mingine kama vile Mwanza na KILImanjaro wametumia Sheria zile zile na wamefanikiwa kuiweka Miji yao katika usafi kwa nini Tabora washindwe.
Balozi Dkt. Batilda alisema Mkoa wa Tabora una historia kubwa kwa Tanzania ni lazima uwe mfano mzuri katika vitu vyote ikiwemo suala la kuwa na miji iliyo safi na inayovutia,
Mkuu huyo wa Mkoa alisema Ofisi yake itaanzisha mashinda kwa Wilaya zote na kutoa tuzo kwa itakayofanya vizuri katika utunzaji wa mazingira na usafi.
Aidha Balozi Dkt. Batilda alimpongeza Mkuu wa Wilaya ya Tabora Dkt. Yahya Nawanda kwa kuanzisha kampeni ya kushiriki usafi katika maeneo ya soko.
Naye Dkt. Nawanda alisema wamejipanga kuendesha opesheni ya kusafisha mji huo na kuondoa takataka katika maeneo yote na kuzipeleka sehemu ya kuziteketeza.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Balozi Dkt.Batilda Buriani (katikati) akitoa jana hotuba ya kuzindua Baraza la Biashara la Manispaa ya Tabora.
Mkuu wa Wilaya ya Tabora Dkt. Yahya Nawanda akifungua jana kikao cha uzinduzi wa Baraza la Biashara la Manispaa ya Tabora
Baadhi ya Wajumbe wa Baraza la Biashara la Manispaa ya Tabora wakifuatilia hotuba ya uzinduzi wa Baraza la leo.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Balozi Dkt.Batilda Buriani ( kushoto ) akibadilishana mawazo na Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Dkt. Isac Laizer (katika) mara baada ya kuzindua jana Baraza la Biashara la Manispaa ya Tabora
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Taborra Ramadhani Kapera akitoa maneno ya utanguzi jana wakati wa uzinduzi wa Baraza la Biashara la Wilaya ya Tabora.
0 Comments