Na Anthony Ishengoma-Shinyanga
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Philemon Sengati amesema michezo inapotumika vizuri inaweza kuwa motisha kubwa sana katika suala zima la ustawi na maendeleo ya jamii.
Dkt. Sengati alisema hayo jana alipoweka jiwe la Msingi katika vyumba viwili vya madarasa vyenye thamani ya 40M/= za kitanzania vinavyojengwa katika Shule ya Msingi Nyakahanga Manispaa ya Kahama vilivyoanzishwa na mashabiki wa Simba na Yanga wanaoishi na kufanya kazi Manispaa ya Kahama.
Dkt. Sengati aliwasifu mashabiki hao ambao walitumia nguvu yao kwa kushirikiana na wananchi na hatimaye kuanzisha vyumba hivyo ambavyo viko katika hatua za mwisho kukamilika kwa nyongeza ya fedha ya serikali kwa kutumia mapato ya ndani.
Aidha Dkt. Sengati amewataka wananchi na viongozi wa Manispaa ya Kahama kusimamia ubora katika ujenzi na kuwaomba kukamilisha mradi huo kwa wakati na kusema hicho ndicho kinachotakiwa katika kuharakisha maendeleo ya serikali.
Naye Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Nyakahanga akisoma taarifa ya Shule kwa Mkuu wa Mkoa alisema kuwa ujenzi wa vyumba hivyo vya madarasa utasaidia kuboresha mazingira mazuri ya kujifunza na kujifunzia kwa kupunguza msongamano wa wanafunzi shuleni hapo.
Wakati huo huo Afisa Elimu Msingi wa Manispaa ya Kahama Bi. Amida Kaganda aliongeza kuwa yeye na watumishi wenzake waliweza kwa kushirikiana na wananchi wa Nyakahanga kusaidina na mashabiki hao wa Simba na Yanga kuanzisha ujenzi wa Vyumba hivyo.
Aidha Bi. Kaganda aliongeza kuwa pamoja na uwepo wa fedha lakini watumishi pamoja na wananchi walichangia katika kusafisha eneo pamoja na kufanya usafi na hatimaye kutoa mchango mkubwa katika kuwezesha ujenzi wa vyumba hivyo hapo Shuleni.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Philemon Sengati akikata utepe kuweka jiwe la Msingi kwa vyumba vya madarasa vya Shule ya Msingi Nyakahaga ya Kahama vyumba vilivyoanzishwa na Masahabiki wa Simba na Yanga.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Philemon Sengati akiongea na Jumuiya ya shule baada ya kukata utepe kuweka jiwe la Msingi kwa vyumba vya madarasa vya Shule ya Msingi Nyakahaga ya Kahama vyumba vilivyoanzishwa na Masahabiki wa Simba na Yanga.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Philemon Sengati akiongea na Jumuiya ya shule baada ya kukata utepe kuweka jiwe la Msingi kwa vyumba vya madarasa vya Shule ya Msingi Nyakahaga ya Kahama vyumba vilivyoanzishwa na Masahabiki wa Simba na Yanga.
0 Comments