Ticker

6/recent/ticker-posts

RC SENGATI AWASILISHA TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA ILANI YA CCM MKOA WA SHINYANGA

Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Dkt. Philemon Sengati akitoa taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa Kipindi cha Mwezi Januari hadi Juni 2021 kwenye Kikao Maalumu cha Halmashauri Kuu CCM Mkoa wa Shinyanga leo Jumatano Agosti 18,2021 katika Ukumbi wa CCM Mkoa wa Shinyanga.

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Dkt. Philemon Sengati amesema Serikali ya Mkoa wa Shinyanga inaendelea kusimamia na kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kufanya mambo yanayoonekana katika jamii ili kuhakikisha kura za uchaguzi zinaenea katika uchaguzi Mkuu ujao.

Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Dkt. Philemon Sengati ameyasema hayo leo Jumatano Agosti 18,2021 wakati akitoa taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa Kipindi cha Mwezi Januari hadi Juni 2021 kwenye Kikao Maalumu cha Halmashauri Kuu CCM Mkoa wa Shinyanga kilichofanyika katika Ukumbi wa CCM Mkoa wa Shinyanga.

"Serikali ya mkoa wa Shinyanga kwa kushirikiana na Chama cha Mapinduzi itaendelea kusimamia utekelezaji wa Ilani ya CCM ili kuhakikisha kura za uchaguzi zinaenea katika uchaguzi Mkuu ujao mwaka 2025", amesema Dkt. Sengati.

"Hatutakuwa legelege katika kusimamia Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020 - 2025, tutakuwa imara ili kutimiza maono yaliyopo katika Ilani ya CCM tunayafikia ili kuleta uhalali wa mambo mazuri ya maendeleo yanayofanywa na serikali ya Chama Cha Mapinduzi machoni pa Watanzania. Nasisitiza pia viongozi wa Chama wapewe kipaumbele wanapofika katika ofisi za serikali",ameeleza Dkt. Sengati.

Mkuu huyo wa mkoa amesema mkoa wa Shinyanga bado una maeneo mengi ya uwekezaji wa viwanda, hivyo kuwaribisha wawekezaji kuja kuwekeza yakiwemo maeneo ya kimkakati huku akibainisha kuwa shughuli za uchimbaji madini ya Almasi katika mgodi wa Williamson Diamond Ltd 'Mgodi wa Mwadui' zimeanza baada ya kusimama.

"Wakati mgodi wa dhahabu wa Buzwagi uliopo Kahama unapoelekea kufungwa tumeelekeza wajenge uwanja wa Ndege uliopo katika mgodi huo uwe wa kisasa na wajenge soko la kisasa kwa ajili ya uchumi endelevu wa Kahama na mkoa kwa ujumla",amesema Dkt. Sengati.

Aidha amesema serikali inaendelea kufuatilia na kuwakamata wezi wa dawa za serikali, kuboresha huduma za afya zikiwemo bima ya afya, mapambano dhidi ya VVU na UKIMWI na kupunguza vifo vya mama na mtoto.

"Hali kadhalika tunaendelea na ukusanyaji mapato, usambazaji umeme na maji vijijini, kujenga miundo mbinu ya barabara, upimaji ardhi ambapo mpaka sasa jumla ya viwanja 101,000 vimepimwa na zoezi la utoaji hatimiliki linaendelea",amesema.

Katika hatua nyingine amesisitiza umuhimu wa kupanda miti ili kutunza mazingira huku akionya ukataji hovyo wa miti katika wilaya ya Kishapu.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga Mhe. Mabala Mlolwa amesema ni vyema viongozi wa CCM na wanachama wa CCM wakashirikiana na viongozi wa serikali wakiwemo wakuu wa wilaya katika kutekeleza Ilani ya uchaguzi wa CCM.

Mlolwa amezitaka mamlaka zinazohusika na ukusanyaji mapato kwenda kukusanya kodi/mapato kwa njia za halali huku akionya halmashauri za wilaya zinazosababisha hati chafu kuacha uzembe kwani zinaharibu sifa ya halmashauri, mkoa na Chama Cha Mapinduzi.

"Kwenye suala la mapato hakuna kuvumiliana. Hatutegemei kusikia halmashauri imepata hati chafu wala hati yenye mashaka. Naomba wenyeviti wa halmashauri muwe wakali sana. Hati chafu zinatuumiza, mtu anasababisha hati chafu halafu baadae unasikia kahamishiwa mkoa mwingine, sisi tunabaki na aibu ya hati chafu",amesema Mlolwa.

Wajumbe wa Halmashauri Kuu CCM Mkoa wa Shinyanga wameipokea taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa Kipindi cha Mwezi Januari hadi Juni 2021 iliyowasilishwa na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Philemon Sengati.

ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Dkt. Philemon Sengati akitoa taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa Kipindi cha Mwezi Januari hadi Juni 2021 kwenye Kikao Maalumu cha Halmashauri Kuu CCM Mkoa wa Shinyanga leo Jumatano Agosti 18,2021 katika Ukumbi wa CCM Mkoa wa Shinyanga
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga Mhe. Mabala Mlolwa akifungua Kikao Maalumu cha Halmashauri Kuu CCM Mkoa wa Shinyanga cha Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa Kipindi cha Mwezi Januari hadi Juni 2021 leo Jumatano Agosti 18,2021 katika Ukumbi wa CCM Mkoa wa Shinyanga
Kikao Maalumu cha Halmashauri Kuu CCM Mkoa wa Shinyanga cha Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa Kipindi cha Mwezi Januari hadi Juni 2021 kikiendelea katika Ukumbi wa CCM Mkoa wa Shinyanga

Post a Comment

0 Comments