Na Anthony Ishengoma
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Philemon Sengati ameyataja mawasiliano afifu kati ya Ofisi za Halmashauri na Ofisi ya Mkaguzi wa Hesabu za Serikali kuwa moja ya chanzo kilichopelekea baadhi ya Halmashauri mkoani Shinyanga kupata hati chafu na zenye mashaka zilizotolewa na ofisi hiyo kwa mwaka wa fedha 2020.
Dkt. Philemon Sengati aliongeza kuwa Halmashauri hizo zilishindwa kufanyia kazi baadhi ya hoja mpya ambazo awali hazikuwemo katika hoja za Ofisi ya Mkaguzi wa Hesabu za Serikali lakini Halmsahauri zikashindwa kuzijibu kwa wakati na kupelekea Halmashauri baadhi ya Halmashauri kupata hati chafu na zenye mashaka.
Dkt. Sengati alisema hayo wakati akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa Ilani Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi kwa kipindi cha Januari hadi Juni 2021 na kuongeza kuhaidi kuwa Mkoa utahakikisha changamoto zilizopojitokeza na kupelekea Halmashauri kupata hoja hazitokei tena.
Dkt. Sengati aidha aliitaja sababu nyingine kuwa ni wahasibu kukosa mafunzo ya ufungungaji hesabu za serikali ikiwemo namna bora ya uhandishi wa taarifa ya hesabu za serikali na kuongeza kuwa Mkoa utahakikisha wahasibu hao wanapata mafunzo hayo mara kwa mara kwa lengo la kuboresha ufanisi wao katika kufunga hesabu za serikali.
Naye Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Shinyanga Bw. Mlolwa Mabala wakati wa Majumuisho yake kwa taarifa hiyo aliutaka uongozi wa Mkoa kuahakikisha Halmashauri za Shinyanga hazipata hati chafu kwakuwa suala hilo halileti sifa nzuri kwa mkoa lakini akaonesha imani yake kwa uongozi wa mkoa katika kupambana na changamoto zilizopo.
Aidha Bw. Mabala amaeutaka uongozi wa Serikali Mkoani Shinyanga kuhakikisha unasimamia kwa karibu ujenzi wa Jengo la Halmashauri ya Shinyanga kwa karibu kwani katika ziara yake kukagua miradi hiyo aliona mapungufu kutoka kwa mkandarasi wa jengo hilo ambaye ni SUMA JKT kuwa haweki nguvu kazi ya kutosha na hivyo kuofu kama ujenzi utaendana na kasi inayotakiwa.
Ni katika uchangiaji wa taarifa hiyo Mbunge wa Kahama Bw. Jumanne Kishimba wakati akichangia suala la Afya Mkoani humo alipoomba ufafanunuzi kuhusu suala la wanaume kuongozana na wenzi wao kwenda kiliniki kwani kwa mila za Kisukuma suala hilo linaenda kinyume utamaduni wao.
Akitoa ufafanunuzi juu ya suala hilo Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt Yudas Ndungile alisema kuwa lengo la serikali ni kuongeza upendo kwa wanandoa lakini pia ni kumfanya mwanaume atambue magumu na machungu ambayo mama anayapitia ikiwemo suala zima la kudhibiti maambukizi ya virusi vya UKIMWI.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Philemon Sengati akiwasilish taarifa ya utekelezaji ya Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi kwa viongozi wa Chama na Serikali Mkoa wa Shinyanga jana katika ukumbi wa Ofisi ya Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Shinyanga.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi wa Mkoa wa Shinyanga Bw. Mlolwa Mabala akitoa majumuhisho yake baada ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga kuwasilisha taarifa ya utekelezaji ya Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi kwa viongozi wa Chama na Serikali Mkoa wa Shinyanga jana katika ukumbi wa Ofisi ya Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Shinyanga.
Wajumbe wa Kamati ya Siasa ya Mkoa wa Shinyanga wakifuatilia jambo wakati Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Philemon Sengati akiwasilisha taarifa ya utekelezaji ya Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi kwa viongozi wa Chama na Serikali Mkoa wa Shinyanga jana katika ukumbi wa Ofisi ya Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Shinyanga.
0 Comments