- RC Makalla afanya kikao site, mkandarasi aridhia kuendelea na Ujenzi.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla amefanikiwa kupatia ufumbuzi hali ya sintofahamu iliyokuwa ikikabili Mradi wa Ujenzi wa Soko la Kisasa la Tandale lenye thamani ya Bilioni 8.7 baada ya Ujenzi huo kusimama kwa muda Kutokana kutoka kile kilichodaiwa kuwa Mkandarasi amecheleweshewa malipo.
Mapema leo RC Makalla amekagua Mradi huo na kufanya kikao Cha kutegua kitendawili kilichokuwepo ambapo kikao hicho kimekuwa na Mafanikio makubwa.
Miongoni mwa maazimio ya kikao hicho ni Mkandarasi kukubali kuendelea na kazi ambapo ameahidi kuwa ifikapo January 31 mwakani Mradi utakuwa umekamilika na kukabidhiwa.
Aidha RC Makalla amesema atafanya ufuatiliaji wa fedha za Mkandarasi zipatikane kwa wakati ili Hali hiyo isijirudie tena ambapo amemuelekeza Katibu tawala wa Mkoa na Manispaa ya Kinondoni kuhakikisha wanashughulikia madai ya Mkandarasi.
Hata hivyo RC Makalla amesema kupitia meza ya maridhiano Mkandarasi amekubali kupunguza madai alilokuwa akidai kutoka Shilingi Milioni 664 hadi 265 sawa na 40% ambapo amempongeza Mkandarasi kwa kuonyesha uzalendo huo.
Itakumbukwa kuwa Agost 11 mwaka huu, Kitibu Mkuu wa CCM Daniel Chongolo alitembelea Mradi huo ambao ulianza September 09/2019 na ulipangwa kukamilika September 13/ 2020 lakini Kutokana na changamoto za malipo Mradi huo haujakamilika adi Sasa Jambo lililomlazimu kutoa maelekezo ya kupatiwa ufumbuzi.
0 Comments