Ticker

6/recent/ticker-posts

RC DKT SENGATI AIZUIA BUZWAGI KUAMISHA MALI MGODINI APANGA KUUNDA TUME KUCHUNGUZA MIRADI



Na Anthony Ishengoma –Shinyanga



Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt.Philemon Sengati ameutaka mgodi wa Buzwagi ambao tayari umesimamisha shughuli zake kutoamisha mali zozote kutoka ndani ya mgodi wala kufungua mitambo ya uchenjuaji madini mpaka Kamati ya Taifa ya Ufungaji Mgodi itakapojilidhisha na kufikia muafaka .



Dkt.Sengati aliiambia Managementi ya Mgodi mbele ya wajumbe wa Kamati ya Taifa ya Ufungaji Mgodi wa Buzwagi kuwa Kamati hiyo unazingatia uwepo wa muafaka mzuri ambao unazingatia maslahi mapana ya serikali na kutaka vyombo vya ulinzi kusimamia zoezi hilo mpaka kamati na mgodi watakapofikia muafaka.



Dkt Sengati alisema hayo wakati yeye na Kamati ya Taifa ya Kufunga mgodi walipotembelea miradi ambayo mgodi huo umehaidi kutekeleza kama faida ya uwepo mgodi huo kwa jamii na kubaini miradi hiyo ni miradi bubu ambayo ipo kuwadaa wananchi na serikali.



‘’Nawataka kutojikita katika kuhamisha mali za mgodi kwasababu suala hilo lipo kisheria na kuonya kuwa kama watakiuka agizo lake serikali iko macho na watachukuliwa hatua’’. Alionya Dkt Sengati Mkuu wsa Mkoa wa Shinyanga.



Katika hatua nyingine Dkt.Sengati amesema ataunda tume kuchunguza matumizi ya fedha za miradi yaliyotengwa kwa ajili ya utekelezaji wa miradi hiyo ambayo inaonekana na miradi isiyokidhi thamani ya fedha iliyotajwa baada ya kupata taarifa kutoka kwa Kamati kuwa Mgodi umetenga dora milioni 1.1 kwa ajili ya mradi wa Kilimo lakini uwekezaji katika mradi huo haundani na thamani ya fedha hiyo.



Suala hilo likamsukuma Dkt. Sengati kuunda Tume ya kuchunguza thamani ya fedha iliyotolewa kwa miradi yote iliyo chini ya mradi huo ikiwemo mradi wa ufugaji nyuki na Skimu ya Umwagiliaji na tume hiyo itaundwa na wataalam wa fedha, Takukulu na vyombo vya usalama kwa lengo la kujiridhisha na kama itabainika kuna ubadhilifu hatua za kisheria zitachukuliwa.



Mradi huo awali uliozinduliwa na Kiongozi wa mbio za Mwenge mwaka huu Luteni Josephine Mwambashi ambao baada ya Kamati kuukagua amegundua haundani na kiasi cha rasimali fedha kilichotolewa na mgodi huo .



Mkurugenzi wa Manispaa ya Kahama Bw. Anderson Nsumba aliiambia kamati hiyo kuwa mgodi ulikataa kufuata mpango ambao Halmashauri iliwasilisha kwao baada ya Tume ya Taifa ya Umwagiliaji kusanifu mradi huo na kupendekeza kuwa utekelezaji wake ungegharimu kiasi cha Tsh. Bilioni kumi lakini Buzwagi wanataka kutekeleza mradi huu kwa kiasi cha milioni 700 na kulingana na ukubwa wa eneo fedha hizo haziwezi kuleta tija.



Kamati hiypo pia ilitembelea uwanja wa ndege wa Buzwagi ambao kwa kipindi kirefu umekuwa ukitumiwa na Mgodi ambao kwa sasa uko katika hali mbaya kutokana na kuchakaa hali iliyomsukuma Dkt. Sengati kuangazia suala la uwanja huo.



Dkt. Sengati akautaja uwanja huo kuwa wa umuhimu kwa uchumi wa Kahama hivyo ni vyema Manegimenti ya Mgodi ikashauriwa kuhusu matengenezo yake na kuongeza kuwa ingekuwa vyema wakawekeza katika miradi yenye tija badala ya kuwekeza katika miradi mingi midogo midogo ambayo haina maana kwa jamii. Meneja wa Mgodi huo Bi.Rebeka Stivin aliimbia kamati hiyo kuwa uwanja wa ndege hauko tena mikononi mwao kwani tayari wamedhakabidhi mamlaka za viwanja vya ndege Nchini lakini kamati hiyo ilioendekeza ukarabati huo ni bora ukakarabatiwa na Mgodi kwa kuwa taratibu za kufunga Mgodi bado zinaendelea chini ya Kamati hiyo.



Aidha mgodi wa Buzwagi unataka kukarabati tu jengo la abiria wakati njia ya kurushia ndege ikiwa imejaa mashimo na kwa mujibu wa Manispaa ya Kahama gharama za ukarabati uwanja huo ni takriban bilioni 4.



Naye Bi. Sundi Malomo kutoka Time ya Taifa ya madini amlisema kuwa Sheria iko wazi kwamba mwekezaji anapotaka kutoka lazima aangalie namna ya kuilinda jamii namna ya kuishi akiutaka uongozi wa Mgodi kuangalia upya bajeti yao ili mradi uweze kutekelezeka.



Kamati hiyo umekuwa katika Majadiliano ya Siku tatu na Utawala wa Mgodi huo na Kamati hiyo imeutaka Utawala wa Mgodi kuheshimu makubaliano yatokanayo na Majadiliano hayo ikiwemo yale ya vikao vya awali.


Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Philemon Sengati akiongoza wajumbe wa Kamati ya Taifa ya Ufungaji Mgodi katika majadiliano ya ufungaji mgodi huo juzi katika ofisi za mgodi huo Buzwagi Kahama mkoani Shinyanga.

Meneja wa Mgodi wa Buzwagi Bi. Rebeka Stivini akiwasilisha mada kwa Kamati ya Taifa ya Ufungaji mgodi mapema jana wakati wa majadiliano ya ufungaji mgodi huo juzi katika ofisi za mgodi huo Buzwagi Kahama mkoani Shinyanga.

Wajumbe wa Kamati ya Taifa ya Ufungaji Mgodi wakikagua Skimu ya Umwagiliaji ambayo inatarajiwa kufadhiliwa na Mgodi wa Buzwagi iliyoko nje kidogo ya Manispaa ya Kahama.

Post a Comment

0 Comments