Ticker

6/recent/ticker-posts

RAIS DKT. MWINYI AJUMUIKA NA WANANCHI KATIKA SALA YA KUUSALIA MWILI WA MAREHEMU YAHYA ABDULWAKIL


RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi akimfariji na kumpa pole Mbunge wa Jimbo la Kwahani Zanzibar Mhe. Ahmad Yahya Abdulwakil kwa kufiwa na Baba yake mzazi Marehemu Yahya Abdulwakil, wakati akiwasili katika Masjid Ameirtajo Mpendae Wilaya ya Mjini Unguja, kuhudhuria maziko na Ibada ya Sala ya Ijumaa iliofanyika katika Masjid hiyo.(Picha na Ikulu)

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi akijumuika na Waumini wa Dini ya Kiislam katika Ibada ya Sala ya jeneza kuusalia mwili wa marehemu Yahya Abdulwakil, Baba Mzazi wa Mbunge wa Jimbo la Kwahani Zanzibar (kushoto kwa Rais) Mhe. Ahmada Yahya Abdulwakil,Makamu wa Pili wa Rais Mstaafu. Alhaj Balozi Seif Ali Iddi na Naibu Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh.Mahmoud Mussa Wadi na (kulia kwa Rais) Rais Mstaafu wa Zanzibar Alhaj Dk. Ali Mohamed Shein na Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar. Mhe.Zuberi Ali Maulid.(Picha na Ikulu)

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi akifuatilia hutuba ya Ibada ya Sala ya Ijumaa ikisomwa na Khatibu Sheikh. Khalid Ali Mfaume, kabla ya Ibada ya Sala ya Ijumaa iliyofanyika katika Masjid Ameirtajo Mpendae Wilaya ya Mjini Unguja.(Picha na Ikulu)

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi akisalimiana na kuagana na Rais Mstaafu wa Zanzibar Awamu ya Saba Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein, baada ya kumaliza kwa Sala ya kuusalia mwili wa Marehemu Yahya Abdulwakil Baba mzazi wa Mbunge wa Jimbo la Kwahani Zanzibar Mhe. Ahmada Yahya Abdulwakil, iliofanyika katika Masjid Ameirtajo Mpendae Wilaya ya Mjini Unguja.(Picha na Ikulu)

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi, akiitikia dua ya kumuombea Marehemu Yahya Abdulwakil, Baba mzazi wa Mbunge wa Jimbo la Kwahani Zanzibar (kushoto kwa Rais) Mhe.Ahmada Yahya Abdulwakil, Makamu wa Pili wa Rais Mstaafu Alhaj Balozi Seif Ali Iddi na Naibu Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh. Mahmoud Mussa Wadi na (kulia kwa Rais) Rais Mstaafu wa Zanzibar Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein, wakiitikia dua baada ya kumaliza kwa Sala ya kuusalia mwili wa Marehemu, iliofanyika katika Masjid Ameirtajo Mpendae Wilaya ya Mjini Unguja.(Picha na Ikulu)

Post a Comment

0 Comments