RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa amesimama baada ya kuwasili kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, katika ukumbi wa mkutano wa Jakaya Kikwete Ikulu Jijini Dar es Salaam, na (kushoto kwake) Makamu wa Rais wa Tanzania Mhe.Dkt. Philip Isdor Mpango na (kulia kwake) Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa, wakati wa hafla ya kukabidhi Taarifa ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania uliofanyika mwaka jana 2020.(Picha na Ikulu)
MWENYEKITI wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Tanzania (NEC) Mhe. Jaji Rufaa (Mst) Semistocles Kaijage,akiwasilisha Ripoti ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania uliofanyika Mwaka 2020, wakati wa hafla ya kukabidhi ripoti hiyo kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan.(kushoto) na (kulia) Makamu wa Rais wa Tanzania Mhe.Dkt.Philip Isdor Mpango na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi, wakifuatilia ripoti hiyo, ikiwasilishwa katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Ikulu Jijini Dar es Saaam.(Picha na Ikulu)
/RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akifuatilia hutuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan.(hayupo pichani) akizungumza baada ya kukabidhiwa kwa Ripoti ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania kwa mwaka 2020, na(kushoto kwake) Makamu wa Rais wa Tanzania Mhe.Dkt.Philip Isdor Mpango na (kulia kwake) Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan akihutibia katika hafla ya kukabidhiwa kwa Ripoti ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania uliofanyika mwaka jana 2020, hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Ikulu Jijini Dar es Salaam.(Picha na Ikulu)
WAJUMBE wa Tume ya Uchaguzi ya Taifa Tanzania na Wageni waalikwa wakifuatilia hutuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan.(hayupo pichani) wakati wa kukabidhiwa kwa Ripoti ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania uliofanyika mwaka jana 2020, hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete Ikulu Jijini Dar es Salaam.(Picha na Ikulu)
0 Comments