Ticker

6/recent/ticker-posts

NAIBU WAZIRI WA AFYA AHIMIZA CHANJO KWA WANANDOA

Na Mwandishi Wetu Songea

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Mwanaidi Ali Khamis amewahimiza wananchi kujitokeza kwa hiari na kupata Chanjo ya UVIKO19 hasa Wazee kwa kuwa salama na imethibitishwa na Watalaam wa Afya. Mwanaidi ametoa kauli hiyo Wilayani Songea Mkoani Ruvuma wakati wa ziara yake mkoani humo kukagua huduma za matibabu kwa Wazee katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa. Amewataka Maafisa Ustawi wa Jamii na Maafisa Maendeleo ya Jamii kuendelea kutoa elimu na kuwahamasisha Wazee kuanzia umri wa miaka 50 kujitokeza kwa hiari yao kupata Chanjo ya UVIKO19. "Awamu hii ya utoaji wa Chanjo ya UVIKO19 tumewapa kipaumbele Wazee kuanzia miaka 50 kupata Chanjo ya UVIKO19 ili kusaidia kupata kinga itakayowalinda na maambukizi ya Virusi vya Corona" alisema Mhe. Mwanaidi Aidha, Mhe. Mwanaidi amewahimiza wanandoa walio na umri wa miaka 50 na kuendelea kuhimizana kupata Chanjo ya UVIKO19 ili waweza kujikinga na Virusi vya Corona.

Kwa upande wake Afisa Maendeleo ya Jamii Mkoa wa Ruvuma Mariam Juma amesema kuwa wataendelea kuhamasisha jamii hasa kundi la wazee na watu wenye magonjwa sugu kujitokeza kwa hiari yao kupata Chanjo ya UVIKO19. Wakati huo huo Mhe. Mwanaidi Ali Khamis ameuagiza uongozi wa Hospitali ya Rufaa ya  Mkoa wa Ruvuma kuhakikisha wanaweka utaratibu mzuri wa kuwahudumia Wazee wanaokuja kupatiwa huduma Hospitalini hapo.

Naibu Waziri Mhe. Mwanaidi pia ametembelea Chuo Maendeleo ya Jamii Mlale na kujionea jinsi Chuo hicho kinavyoshirikiana na wananchi kuleta mawazo ya kibunifu yanayosaidia kutatua changamoto mbalimbali katika jamii.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Mwanaidi Ali Khamis akizungumza na Mzee Florian Mbilinyi aliyekuwa akipatiwa huduma katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Ruvuma.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Mwanaidi Ali Khamis akipatiwa Chanjo ya UVIKO19 katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Ruvuma  ikiwa sehemu ya uhamasisishaji Jamii hasa Wazee kupata Chanjo hiyo.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Mwanaidi Ali Khamis akikabidhi malighafi ya kutengeza vikapu kwa Kikundi cha Wanawake wajasirimali cha Malkia wa Nguvu kilichopo Manispaa ya Songea mkoani Songea.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Mwanaidi Ali Khamis akiangalia mashine iliyobuniwa na mmoja ya Wakazi itakayotumika kusambaza maji katika vijiji vinavyozunguka Chuo cha Maendeleo ya Jamii Mlale.

Post a Comment

0 Comments