Na Alex Sonna,Mbeya
MWANAFUNZI wa kidato cha nne katika shule ya Sekondari ya Ufundi ya Iyunga ya Mkoani Mbeya,Yusuph Ng'umbi amebuni kifaa kiitwacho Public Area Accounter ambacho kitasaidia kukusanya mapato katika maeneo ya wazi yenye shughuli za kijamii.
Akizungumza na Waandishi wa Habari leo, Agosti 20,2021, waliofika shuleni hapo kuangalia ubunifu unaofanywa na wanafunzi wa shule hiyo, mwanafunzi huyo amesema kifaa wamekitengeneza ili kiwe na uwezo wa kusimamia sehemu ambazo kuna ukusanyaji wa fedha.
Mfumo wetu tumeutengeneza kwa sababu sio wote ambao wanakusanya mapato ni waaminifu baadhi yao huwa wanachukua kiasi cha hela na kupunguza mapato katika serikali.
"Sasa huu mfumo wetu tumeutengeneza ambapo mkusanyaji akiishakusanya hela mtu akipita katika hilo eneo atahesabiwa na kuonekana mtu mmoja amepita na itahesabu hela aliyotoa.
Amesema Baada ya hapo mwisho wa siku itajumlisha watu waliopita na kiasi kilichopatikana na kutuma taarifa makao makuu au kwa mtu binafsi au katika Halmashauri.
ALIPOLIPATA WAZO
Mwanafunzi huyo amesema wazo hilo alilipata wakati akiwa kituo cha basi na rafiki zake ambapo walianza kubishana kwamba fedha ambazo zimekuwa zikikusanywa katika vyoo vya kulipia hazifiki katika Halmashauri zote kwani baadhi wamekuwa wakijinufaisha.
“Wazo hilo lilikuja kipindi cha Corona nilikuwa na marafiki zangu tukiwa kituo cha basi tukawa tunabishana kuhusiana na vyoo vya kulipia tukajadiliana kwamba jamaa hapeleki hela kamili katika Halmashauri kwahiyo tuliporudi mwezi wa sita tukaanza kulifanyia kazi,”amesema
ATUMIA MIEZI SITA KUTENGENEZA
Amesema ametumia miezi sita kukamilisha Project hiyo ambapo walipofika wataalamu wa Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia waliipeleka katika Mashindano ya Taifa ya Sayansi Teknolojia na Ubunifu (MAKISATU) Mkoani Dodoma.
“Huu mfumo tumeutengeneza uwe unakaa sehemu uliyojificha hata msimamizi hawezi kujua na hawezi kujua sehemu gani umekaa na tumeweka mfumo huu mtu asiweze kuingilia na kuuchezea,”amesema
WAISHUKURU WIZARA YA ELIMU,SAYANSI NA TEKNOLOJIA
Kwa upande wake Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Ufundi Iyunga Edward Mwantimwa ametoa shukrani kwa Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia kwa kuwaendeleza wabunifu katika shule za Sekondari.
Amesema shule hiyo imekuwa ikitoa wanafunzi wenye vipaji ikiwemo mwanafunzi aliyebuni kifaa cha kukusanya mapato katika Halmashauri
“Wanafunzi wamefanya ubunifu kupata uhalisia wa mapato kama kiingilio madhalani katika Standi,sokoni akitaka kujua wanachaji shilingi ngapi anamweka mtu kutokana na uaminifu wake, mfumo huu unaweza kutatua changamoto.
“Pia jinsi gani rahisi ya kuweza kupata uhalisia wa mapato yanayopatikana katika kuchaji hasa katika kiingilio madhalani Sokoni anataka kujua anachaji shilingi ngapi lakini anamweka mtu ambaye inategemea uaminifu wake,” amesema
MWANAFUNZI wa kidato cha nne katika shule ya Sekondari ya Ufundi ya Iyunga ya Mkoani Mbeya,Yusuph Ng'umbi,akizungumza na wanadishi wa habari waliofika shuleni hapo kuangalia ubunifu unaofanywa na wanafunzi wa shule hiyo,
MWANAFUNZI wa kidato cha nne katika shule ya Sekondari ya Ufundi ya Iyunga ya Mkoani Mbeya,Yusuph Ng'umbi,akiwaonyesha wanadishi wa habari waliofika shuleni hapo kuangalia ubunifu unaofanywa na wanafunzi wa shule hiyo,kifaa kiitwacho Public Area Accounter ambacho kitasaidia kukusanya mapato katika maeneo ya wazi yenye shughuli za kijamii.
Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Ufundi Iyunga Edward Mwantimwa,akitoa shukrani kwa Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia kwa kuwaendeleza wabunifu katika shule za Sekondari.
0 Comments