********************************
Nteghenjwa Hosseah, Sengerema
Waziri wa Nchi @ortamisemitz Mhe @ummymwalimu amesema Serikali itapeleka Shilingi Milioni 450 kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa maboma 6 ya madarasa ya shule za msingi, 6 sekondari na Maboma 6 ya Zahanati yaliyowasilishwa @ortamisemitz.
Waziri Ummy ameyasema hayo wakati wa ziara yake Wilayani humo kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
Amesema @ortamisemitz kwa mwaka wa Fedha 2021/22 tumetenga shilingi mil 12.5 kwa kila Boma la Darasa lililoanzishwa kwa nguvu za wananchi na kufikia kwenye Lenta na Milioni 50 kwa kila Zahanati iliyoanzishwa na Wananchi na kufikia kwenye hatua ta Lenta ili kuunga mkono juhudi za wananchi kukamilisha maboma hayo yaanza kutoa huduma.
Mhe. @ummymwalimu akiwa katika Shule ya Msingi Kachuho Wilayani Sengerema amesema Shule hiyo itapelekewa shilingi Mil 25 ili kukamilisha Ujenzi wa maboma mawili ya madarasa ambayo yameanzishwa kwa nguvu za Wananchi.
0 Comments