*******************************
Katibu mkuu wa chama cha Mapinduzi Daniel Chongolo ameipongeza TANROAD kwa usimamizi mzuri wa mradi wa Ujenzi wa daraja la Tanzanite awali likifahamika kama Daraja la Salenda, ikiwa ni pamoja na kujumuisha wakandarasi wengi wazawa huku akitoa maelekezo kuwa ni muda muafaka sasa kuwepo na program maalum ya kukuza na kuwajengea uwezo wakandarasi wazawa ili fursa za kandarasi zinazoendelea za ujenzi hapa nchini baadae ziweze kufanywa na wazawa.
Ameyasema hayo, leo alipotembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa daraja la Tanzanite katika ziara iliyojumuisha wajumbe wote wa Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa.
Awali akiwasilisha taarifa ya mradi huo, Mtendaji Mkuu wa Tanroad Mhandisi Rogatus Mativila, ameeleza kuwa, ujenzi huo wa daraja umegharimu kiasi cha shilingi Bilioni 243.7 na ukijumuisha asilimia 92 ya wafanyakazi wazawa huku ukitarajiwa kukamilika mwezi Desemba mwaka huu na mpaka sasa umefikia asilimia 91 kukamilika.
0 Comments