Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango akisaini kitabu cha Maombolezo nyumbani kwa aliyekuwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Elias John Kwandikwa , Kibaha Picha ya Ndege mkoani Pwani. Pembeni ni Mke wa Makamu wa Rais Bi. Mbonimpawe Mpango. Agosti 4,2021.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango akimfariji mke wa marehemu Elias John Kwandikwa aliyekuwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Bi. Marceline Kwandikwa pamoja na mtoto wa Marehemu (Kushoto) Jackline Kwandikwa Wakati alipofika kuwapa faraja familia hiyo nyumbani kwa marehemu Kibaha Picha ya Ndege mkoani Pwani. Agosti 4,2021
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango akizungumza na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson Mwansansu wakati alipofika nyumbani kwa marehemu Elias Kwandikwa aliyekuwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Kibaha Picha ya Ndege mkoani Pwani. Agosti 4, 2021.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango akizungumza na waombolezaji waliojitokeza nyumbani kwa marehemu Elias Kwandikwa aliyekuwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Kibaha Picha ya Ndege mkoani Pwani. Agosti 4, 2021.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa Usalama wa Taifa Diwani Athuman Msuya mara alipowasili kuwapa pole kufuatia kifo cha kaka wa Mkurugenzi huyo Bw. Bisward Msuya kilichotokea Agosti 3, 2021.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango Akimfariji Bi. Lisa Msuya ambaye ni mke wa marehemu Bisward Msuya mara alipofika kuitembelea familia hiyo eneo la Tangi Bovu jijini Dar es salaam. Agosti 4, 2021.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango akizungumza na waombolezaji waliojitokeza nyumbani kwa marehemu Bisward Msuya ambaye ni kaka wa Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa Diwani Athuman Msuya. Agosti 4, 2021.
PICHA – OFISI YA MAKAMU WA RAIS
0 Comments