********************************
Jeshi la polisi limefanya operasheni Maalumu ya ukaguzi katika maeneo yaliyokuwa maficho ya wahalifu wenye kujihusisha na matukio ya unyanganyi wa kutumia silaha na matukio yenye mrengo wa kigaidi katika Mkoa wa Kipolisi Rufiji.
Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dodoma Msemaji wa Jeshi la polisi makao makuu ya polisi Jijini humo, SACP David Misime amesema kazi kubwa ilifanywa katika kipindi hicho na jeshi la polisi kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama na wananchi na mafanikio makubwa ya kuwakamata wahalifu pamoja na silaha nyingi zikiwemo za kivita na hali ikarejea kuwa shwari na wananchi kuweza kuendelea na shughuli zao za kujileta maendeleo bila hofu.
'baada ya operasheni hiyo kubwa na hali ya amani na usalama kurejea, jeshi la polisi liliona umuhimu wa kufanya operasheni ya ukaguzi wa maeneo yaliyokuwa yanatumiwa na wahalifu kwa kipindi hicho yakiwepo eneo la wilaya ya Kibiti kama vile Rungungu na Nyambunda". Amesema SACP Misime.
Aidha SACP Misime amesema Jeshi la Ppolisi limeendelea kusisitiza umuhimu wa kila Mtanzania kufuata sheria, kanuni na taratibu za nchi na anayekwenda kinyume tutamchukulia kuwa lengo lake ni kuvuruga amani na utulivu na hatutasita kumchukulia hatua stahiki kwa mujibu wa sheria
0 Comments