Ticker

6/recent/ticker-posts

JATU PLC YAFANIKIWA KUKUSANYA ZAIDI YA SHILINGI BILIONI 7

Mkurugenzi Mtendaji wa JATU PLC Bw.. Peter Isare akizungumza  na wadau wa Kilimo katika mkutano Mkuu wa Wakulima wa JATU PLC uliofanyika katika ukumbi wa Mkutano Ubungo Plaza Jijini Dar es Salaam ambapo alitoa matokeo ya hisa walizoingiza sokoni. Wadau wa Kilimo wakifuatilia wakiwa katika mkutano Mkuu wa Wakulima wa JATU PLC uliofanyika katika ukumbi wa Mkyano Ubungo Plaza Jijini Dar es Salaam.(Picha na Emmanuel Mbatilo)

*********************************

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

Kampuni ya JATU PLC ilikuwa na hisa milioni 15 sokoni ambazo zilitakiwa kuuzwa na kuweza kuleta jumla ya shilingi bilioni 7.5 kwa maana hisa moja ilikuwa inauzwa kwa shilingi 500.

Ameysema hayo leo Mkurugenzi Mtendaji wa JATU PLC Bw.. Peter Isare akizungumza na wadau wa Kilimo katika mkutano Mkuu wa Wakulima wa JATU PLC uliofanyika katika ukumbi wa Mkutano Ubungo Plaza Jijini Dar es Salaam ambapo alitoa matokeo ya hisa walizoingiza sokoni.

Tulifanikiwa kuuza hisa zetu takribani milioni 15,526,372 na kukusanya kiasi cha shilingi Bilioni 7, 723.186,000 ambayo ni sawasawa na asilimia 104% ya zoezi zima .Tumefikia lengo la kuvuka zaidi ya asilimia 4% ya kile ambacho tulikuwa tunakitegemea". Amesema Bw.Isare.

Amesema katika hisa zote hizo watu walionunua hisa ambao si watanzania hawazidi watano kwa maana yake zaidi ya asilimia 99% ya wawezekezaji wa kampuni hiyo ni Watanzania.

"Kwetu hii inafaida kubwa kwasababu pia sisi ndo tunaifahamu kampuni, sisi ndo tunajua inapotoka na inakoenda kwahiyo tunauhakika kwamba yale tuliopanga kuyafanya tutaendelea kuyafanya kwa sababu sisi ndo wamiliki wa kampuni yetu". Amesema Bw.Isare.

Kwa upande wake mwanachama wa JATU PLC Bi.Fatuma Mrutu amesema wamefarijika na matokeo yaliyotokea kwasababu wameweza kupata matokeo mazuri ambayo walitegemea katika kilimo.

Aidha ametoa rai kwa wakulima ambao hawajajiunga na JATU kujiunga na kampuni hiyo  na kuacha kulima wao kama wao kwani kunakuwa na usimamizi mgumu lakini unapokuwa mwananchama wa JATU PLC karibia kila kitu wanafanya wao.

Post a Comment

0 Comments