Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Pauline Gekul leo tarehe 15 Agosti, 2021 ameshirki mbio za hisani za CRDB Marathon zilizokuwa na lengo la kukusanya fedha kwa ajili ya kusaidia upasuaji kwa watoto wenye matatizo ya Moyo kwenye Taasisi ya Jakaya Kikwete.
Mgeni rasmi wa mbio hizo zilizofanyika katika viwanja vya The Green Oysterbay jijini Dar es Salaam, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa pamoja na mambo mengine ameagiza Wizara zinazosimamia michezo kwa watumishi wa Wizara na Idara za Serikali kurejesha michezo ya SHIMIWI.
Mhe. Waziri Mkuu pia ameiagiza wizara ya TAMISEMI kusimamia na kuhakikisha kuwa watumishi pamoja na wanafunzi wanashiriki shughuli za michezo.
0 Comments