Na Alex Sonna,Dodoma
KUNA msemo usemao ‘Chanda chema hivikwa pete’, usemi huu unajidhihirisha kupitia utendani kazi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) iliyoanzishwa kwa mujibu wa Sheria ya Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za nishati na maji ya mwaka 2001.
Mamlaka hiyo imekuwa ikifanya kazi mbalimbali nchini ambapo majukumu yake ni pamoja na kutoa leseni na kusimamia utekelezaji wake, kudhibiti ubora, usalama, na tija ya watoa huduma, kutathmini na kupitisha marekebisho ya bei za huduma, kusikiliza malalamiko na kutatua migogoro na kuelimisha umma kuhusu shughuli za EWURA.
Hivi karibuni EWURA iliandaa semina kwa Taasisi ya Maendeleo ya Viziwi Nchini iliyofanyika Jijini Dodoma ambapo katika wasilisho la Mamlaka hiyo analotoa Meneja wa Mawasiliano na Uhusiano, Titus Kaguo anataja mambo ambayo EWURA inajivunia kupata mafanikio makubwa ni pamoja na uchakachuaji wa mafuta, utatuzi wa migogoro na udhibiti wa sekta ndogo ya gesi asilia.
Washiriki wa mafunzo wakifatilia mada mbalimbali ambazo zilikuwa zikitolewa kwenye emina kwa Taasisi ya Maendeleo ya Viziwi Tanzania(TAMAVITA) iliyoandaliwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) iliyofanyika Julai 20,2021 jijini Dodoma
Mambo mengine ni uagizaji wa mafuta, masharti rahisi ili kuwavutia wawekezaji,jinsi bei za mafuta zinavyopangwa, na utoaji wa leseni.
ILIVYOPAMBANA NA UCHAKACHUAJI WA MAFUTA
Anasema uchakachuaji wa mafuta ni changamoto kubwa hapa nchini ambapo EWURA imepambana na tatizo hili kwani uchakachuaji umepungua kutoka asilimia 80 mwaka 2007 hadi asilimia 4 mwaka 2020.
Kaguo anasema Septemba 2010, EWURA ilianzisha Program ya kuweka vinasaba kwenye mafuta yanayotumika nchini ili kudhibiti ukwepaji kodi (fuel dumping),uchakachuaji na kuweka mazingira ya ushindani wahaki;
Anasema Utafiti wa UDSM kuhusu matumizi ya vinasaba kwamwaka 2010 – 2013 ulibaini ongezeko la mapato yaSerikali (kodi) kwa Shilingi bilioni 468.50 bilion;ikiwa ni Shilingi bilioni 146.5 (2010/11), Shilingibilioni 129.8 (2011/12) na Shilingi bilioni 192.2 (2012/13).
Anasema takribani asilimia 50 ya mafuta yanayoingizwa nchini ni mafuta yanayokwenda nchi jirani (transit) ambapo pia kuna mafuta yenye msamaha wa kodi na uwezekano wa mafuta ya magendo kuingia nchini
Hata hivyo anasema kazi za EWURA ni kuandaa sera,sheria na kanuni zitakazowezesha kukua kwa sekta za nishati na maji na kuendelea kusimamia watoa huduma ili kuhakikisha huduma zinakuwa bora kwa manufaa ya Taifa.
“Hii imesaidia kuzuia mfumuko wa bei,imeimarisha Mamlaka za Maji nchini,imesaidia kukuza umeme binafsi pamoja na mambo mengine mengi.
Kuhusiana na ubora wa miundombinu ya mafuta, Kaguo anasema EWURA inadhibiti ubora wa miundombinu ya mafuta ili kulinda afya, usalama na mazingira na kutokana na udhibiti wa EWURA, maghala na vituo vya mafuta vimeendelea kuwa bora zaidi.
ILIVYOTATUA MIGOGORO
Meneja wa Mawasilino na Uhusiano,huyo anasema EWURA itaendelea kusimamia na kutatua migogoro na malalamiko ya walaji wa huduma zinazodhibitiwa na Mamlaka hiyo dhidi ya watoa huduma.
Anasema Migogoro hiyo inahusu usahihi wa ankara za umeme na maji, kucheleshwa kuunganishiwa huduma za umeme na maji na wananchi kuuziwa mafuta machafu.
Kaguo anasema utatuzi wa migogoro na malalamiko umefanya watoa huduma kuwajibika kuboresha huduma zao.
YAJIVUNIA MAFANIKIO LUKUKI
Anasema katika kipindi cha miaka nane (8) EWURA imechangia Mfuko Mkuu wa Serikali TZS 75.223 Bilioni,EWURA CCC TZS 14.555 Bilion,Baraza la Ushauri la Serikali TZS 5,388 Bilioni,Baraza la Ushindani (FCT) TZS 3217 Bilioni,Tume ya Ushindani (FCC) TZS 957 Milioni.
Kaguo anasema EWURA inaendelea kuwahamasisha wafanyabiashara kuomba leseni za ujenzi wa vituo vya kutolea huduma ya gesi asilia kwa matumizi ya magari
Anasema EWURA imetengeneza kanzi data (database) ya kampuni za wazawa zenye uwezo wa kushiriki kutoa huduma mbalimbali kwenye sekta ya mafuta na gesi asilia.
Anasema hadi kufikia May 31, 2021, kampuni 650 zilishaorodheshwa na wazawa kushika madaraka katika kampuni za gesi asilia.
Aidha, EWURA inaendelea kutayarisha Kanuni na Miongozo mbalimbali ili kusaidia kukuza sekta ndogo ya gesi asilia nchini.
UDHIBITI WA SEKTA NDOGO YA GESI ASILIA
Anasema EWURA imewekeza kwenye utaalam wa gesi asilia kwakuwasomesha watumishi wake, na imekuwa chanzo muhimu cha ushauri wa kitaalamu kwa Serikali
“EWURA imeandaa na kuweka taratibu mbalimbali kama vile utoaji wa leseni wa haraka (miezi 2), kwa uwazi, na ushirikishwaji mpana,uidhinishaji wa mikataba ya kuuziana Umeme (Power Purchase Agreements),uanzishaji wa Mkataba wa Wateja kwaTANESCO (Customer Services Charter),”anasema Kaguo.
KUHUSU VILAINISHI
Meneja huyo anasema EWURA inaendelea kuweka bidii na mkakati mahsusi ili kuboresha uingizwaji, uuzaji na matumizi ya vilainishi bora nchini.
“EWURA itaendelea kutoa elimu kutoa elimu na pia kuchukua hatua za kisheria kwa wanaokiuka sheria na taratibu zilizowekwa.Ni muhimu kufanya biashara ya vilainishi kwa kuzingatia Sheria na Kanuni,”anasema
Anasema changamoto zilizoko katika biashara ya vilainishi zitatatuliwa kwa ushirikiano wa dhati baina ya vyombo vya Serikali (EWURA, TBS, FCC, TRA,Mkemia Mkuu wa Serikali(GCLA), Polisi n.k) nawadau wengine.
Kuhusiana na Uingizwaji wa vilainishi visivyokidhi ubora na Uanzishwaji wa viwanda vya kutengeneza vilainishi pasipo kufuata taratibu na sheria,Kaguo anasema baadhi ya Wafanyabiashara wasio waaminifu ambao wamekuwa wakijaza (repacking) vilainishi visivyokidhi viwango katika vifungashio vya makampuni makubwa yenye chapa zinazoaminika na kuuzwa kwa wingi kwa kusudi la kupata faida kubwa.
Anasema kwa sasa hapa nchini kuna viwanda vinne (4) vinavyozalisha vilainishi ambavyo ni Petrolube, General Petroleum Ltd, Oryx Energies na Tanzania Mineral Oil (Arusha).
“Idadi kubwa ya vilainishi huagizwa kutoka nchi za uarabuni ambako kuna uzalishaji mkubwa wa mafuta. Nchi nyingine: Afrika Kusini, Kenya Vilainishi aina mbalimbali huagizwa kama vile: oili kwa ajili ya injini (engine oils), oili kwa ajili ya gia (gear oils), grisi (grease), coolants, ATF.
Anasema matumizi ya nchi kwa mwaka ni zaidi ya lita milioni 30 za vilainishi. Kiasi kinachozalishwa hapa nchini ni takribani lita milioni 20.
UAGIZAJI WA MAFUTA (BPS)
Anasema EWURA kwa kushirikiana na Wizara ya Nishati iliandaa Mfumo wa Uagizaji wa Pamoja (BPS) wa mafuta nchini.
Anasema Utafiti wa UDSM wa Aprili 2014, ulibaini kuwa, kwa ujumla, BPS imesaidia kupunguza gharama jumla ya Shilingi bilioni 121.57 kwa mwaka kama ifuatavyo:
“Kupungua kwa gharama za usafirishaji (Premium) kwa Shilingi bilioni 81.90 kwa mwaka;kupungua kwa gharama za demurrage kwa Shilingi bilioni 25.72 kwa mwaka;Kupungua kwa gharama za uagizaji mafuta kutokana na maboresho ya mikataba kwa Shilingi bilioni 13.95 kwa mwaka,”anasema.
Anasema faida nyingine za uagizaji wa mafuta kwa pamoja nipamoja nakupatikana kwa taarifa sahihi za kiwango cha mafuta kinachoingizwa nchini na hivyo kuongeza mapato ya kodi ya serikali kwa kiwango cha asilimia 24 kwa mwaka 2012
Pia,kuongeza ufanisi katika udhibiti wa bei za mafuta kwa kuwa na gharama halisi za mafuta yanayoingia nchini.kurahisisha udhibiti wa ubora wa mafuta yanayoingizwa nchini chini ya mfumo huu.
MASHARTI NAFUU KUWAVUTIA WAWEKEZAJI
Anasema EWURA imeandaa masharti nafuu ili kuvutia wawekezaji kwenye maeneo ya vijijini pamoja na kutoa mwongozo wa ujenzi wa vituo vya mafuta vijijini vya gharama nafuu.
“EWURA inashirikiana na wadau mbalimbali kufanya utafiti wa mahitaji ya mafuta vijijini na kubuni kituo cha gharama nafuu muafaka kwa maeneo ya vijijini. Kituo hicho kinaweza kugharimu kati ya Shilingi milion 22.3 mpaka milioni 32.35,”anasema.
JINSI BEI ZA MAFUTA ZINAVYOPANGWA
Anasema bei elekezi zinazopangwa huzingatia gharama za uagizaji,gharama za bandari na taasisi Nyingine,Kodi za Serikali,Gharama za Usambazaji; na Faida kwa wafanyabiashara
Anasema EWURA hufanya ukaguzi wa kushutukiza katika vituo vya kuuzia mafuta na kwa wafanya biashara wa jumla nchini ili kuona kama mafuta yanauzwa kwa bei elekezi.
“Baada ya kuona kuwa bei za mafuta zinapanda kiholela kufikia hata kupandishwa mara tatu kwa siku Januari 2009, EWURA iliingilia kati kwa kuanza kutoa bei kikomo,”anasema.
Anasema kwa kuanza udhibiti wa bei za mafuta mwaka 2009, bei za Dar es Salaam zilishuka kutoka Shilingi 2,000 kwa lita hadi Shilingi 1,233 kwa lita ikiwa ni punguzo la asilimia 62.
Anasema Kwa mikoa ya mbali kama Kigoma, bei ilishuka kutoka takribani Shilingi 2,400 kwa lita hadi Shilingi 1,642 kwa lita ikiwa punguzo la asilimia 52.
“Pamoja na mabadiliko ya bei za mafuta katika soko la dunia na kushuka kwa thamani ya Shilingi dhidi ya Dola ya Marekani, katika kipindi cha miaka 10 tangu EWURA ianze udhibiti wa bei za mafuta, wastani wa bei za mafuta nchini hazijapanda kuzidi bei zilizokuwepo kabla ya EWURA kuingilia katiJanuari 6, 2009,”anasema.
Anasema utafiti uliofanywa na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam uliainisha kuwa udhibiti wa bei za mafuta ulifanikisha kukua kwa pato la ziada la wananchi (disposable income) kwa kiasi cha Shilingi bilioni 445.5 kati ya mwaka 2009 na 2010.
Kaguo anasema udhibiti huo pia uliainisha kuwa udhibiti wa bei za mafuta ulichangia katika kuongeza mapato ya kodi ya Serikali kwa Shilingi bilioni 49 kwa kipindi cha mwaka mmoja tu (Julai 2009 hadi Juni 2010).
UTOAJI WA LESENI
Anasema EWURA inatoa leseni ili kuhakikisha huduma zamafuta zinatolewa kwa kufuata sheria, kanuni na viwango stahiki.
Kaguo anasema hadi kufikia mwezi June 2020, EWURA ilikuwa imetoa leseni 1,515 katika sekta ya mafuta, kati ya
“Hizo,leseni 58 ni za kuuza mafuta kwa jumla,leseni 1,360 za vituo vya mafuta vya rejareja,leseni tano (5) za kuhifadhi mafuta,leseni 50 za biashara ya vilainishi,leseni 18 za kuagiza na kuuza gesi ya kupikia(LPG).
Anasema leseni 2 za kutoa huduma ya mafuta kwenye meli(Bunkering),leseni 15 za kuweka miundombinu binafsi ya kuhifadhia na kujaza mafuta (consumer installations),leseni nne (4) za kusafisha mafuta,leseni moja (1) ya kuchakata mafuta machafu (Waste Oil Recycling) na leseni moja (1) ya kusafirisha mafuta; naleseni moja ya wakala wa uagizaji mafuta kwa pamoja (PBPA).
Meneja Mawasiliano na Uhusiano wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) Bw.Titus Kaguo akiwasilisha mada wakati wa semina kwa Taasisi ya Maendeleo ya Viziwi Tanzania(TAMAVITA) iliyoandaliwa na EWURA ambayo ilifanyika Julai 20,2021 jijini Dodoma.
0 Comments