Ticker

6/recent/ticker-posts

CHELSEA BINGWA UEFA SUPER CUP, YAICHAPA VILLARREAL KWA MIKWAJU YA PENATI 6-5



Mabingwa wa Kombe la klabu bingwa Ulaya UEFA CHAMPION LEAGUE, Chelsea imefanikiwa kuchukua ubingwa wa kombe la Super Cup baada ya kuichapa timu ya Villarreal kwa mikwaju ya penati 6-5 mara baada ya kutoka sare ya bao 1-1.

Chelsea ilianza kupata bao kupitia kwa kiungo wao Hakim Ziyech dakika ya 27 akipokea pasi kutoka kwa mshambuliaji raia wa Ujerumani Kai Havertz.

Chelsea ilikwenda mapumziko ikiwa mbele kwa bao moja na baadae katika kipindi cha pili Villarreal walianza kulisakama lango la Chelsea licha ya kufanya mashambulizi mengi lakini kipa wa  Chelsea Edouard Mendy alionekana shujaa kwenye mechi kwa kuhokoa michomo mingi dhidi ya wachezaji wa Villarreal.

Villarreal ilipata bao la kusawazisha mnamo dakika ya 73 ya mchezo kupitia kwa mshambuliaji wao raia wa Hispania, Gerald Moreno akipokea basi ya kisigino kutoka kwa Boulaya Dia.

 


Post a Comment

0 Comments