Na John Mapepele- WHUSM
Shirikisho
la Mpira wa Miguu wa Barani Afrika (CAF) limepongeza mikakati
inayofanywa na Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan katika kuendeleza
michezo hususan Soka, ambapo wiki ijayo atapokea kombe la CECAFA 2021 la
vijana wenye umri chini ya miaka 23.
Hayo
yameelezwa na Rais wa CAF, Dkt. Patrice Motsepe Agosti 13, 2021
wakati alipokutana na Viongozi Wakuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo, Shirikisho la Soka nchini na Waziri Mkuu, Mhe. Kassim
Majaliwa ambapo amesema timu ya taifa ya Tanzania ina uwezo wa kuwa timu
bingwa barani Afrika kutokana na umahiri iliyonayo sasa.
Aidha ameipongeza Tanzania kuwa nchi ya kuigwa kutokana na wananchi wake wengi kupenda michezo
0 Comments