Ticker

6/recent/ticker-posts

ZIARA YA MHE. MARY MARY MASANJA KUTEMBELEA VIVUTIO VYA UTALII WILAYANI SONGEA


Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) akimsikiliza Mhifadhi wa Makumbusho ya Majimaji na ya Kumbukumbu ya Dkt. Rashid Mfaume Kawawa, Balthazar Nyamusya (kushoto) akitoa maelezo kuhusu zana za mishale zilizotumika kipindi cha vita ya Majimaji, alipofanya ziara ya kikazi ya kukagua eneo la Makumbusho ya  Majimaji lililopo Bombambili Wilaya ya Songea.

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) akimsikiliza Mhifadhi wa Makumbusho ya Majimaji na ya Kumbukumbu ya Dkt. Rashid Mfaume Kawawa, Balthazar Nyamusya (kushoto) akitoa maelezo kuhusu handaki lililopo kwenye Makumbusho ya Dkt. Rashid Mfaume Kawawa  alipofanya ziara ya kikazi ya kukagua eneo hilo lililopo Bombambili Wilaya ya Songea .

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) akimsikiliza Mhifadhi wa Makumbusho ya Majimaji na ya Kumbukumbu ya Dkt. Rashid Mfaume Kawawa, Balthazar Nyamusya (kulia) akitoa maelezo kuhusu mavazi yaliyopo kwenye Makumbusho ya Dkt. Rashid Mfaume Kawawa, wakati wa ziara ya kikazi ya kukagua Makumbusho hiyo iliyopo eneo la Bombambili Wilaya ya Songea.

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) akiangalia mnara wa kumbukumbu  waliponyongwa mashujaa wa Vita vya Majimaji alipofanya ziara ya kikazi ya kukagua eneo hilo lililopo Wilaya ya Songea. Kulia ni Mhifadhi wa Makumbusho ya Majimaji na Makumbusho ya Kumbukumbu ya Dkt. Rashid Mfaume Kawawa, Balthazar Nyamusya.

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) akiongoza msafara kupanda Mlima Matogoro katika Hifadhi ya Misitu ya Milima ya Matogoro iliyopo kwenye Manispaa ya Songea. Nyuma yake ni Kamishna Uhifadhi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) Prof. Dos Santos Silayo.

Post a Comment

0 Comments