Waziri wa Kilimo Mhe. Prof Adolf Mkenda akikagua eneo la kilimo cha Pilipili ambalo lipo chini ya Umoja wa Wajasiriamali wahitimu wa Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUGECO) kwa ajili ya kilimo cha Pilipili katika kijiji cha Luhindo kilichopo katika Wilaya ya Mvomero, Wakati akiwa katika ziara ya kikazi leo tarehe 27 Julai 2021. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
Na Mathias Canal, Wizara ya
Kilimo-Morogoro
Waziri wa Kilimo Mhe. Prof
Adolf Mkenda ameielekeza Tume ya Taifa ya Umwagiliaji kuhakikisha inashirikiana
na Umoja wa Wajasiriamali wahitimu wa Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUGECO)
ili kuimarisha miundombinu ya umwagiliaji kwenye shamba la Pilipili mkoani Morogoro.
Waziri Mkenda ametoa maelekezo
hayo leo tarehe 27 Julai 2021 wakati alipotembelea na kukagua hatua
zilizofikiwa na kusafisha shamba hilo lililopo katika Kijiji cha Luhindo Wilaya
ya Mvomero wakati akiwa katika ziara ya kikazi ya siku moja Mkoani Morogoro.
Pia Waziri Mkenda
amemuelekeza Mkurugenzi Mtendaji wa Tume hiyo kuhakikisha anashiriki kikamilifu
katika usafishaji wa shamba hilo lenye ukubwa wa Hekari 1500 kwa kutumia zana
za kisasa ili kumaliza haraka usafishaji wa shamba hilo.
“Ingekuwa ni vizuri tufanye
kazi hiyo kwa kasi ili kuweza kulima kwa sehemu kubwa na kuongeza uzalishaji
kwa kuwa ardhi ya kutosha ipo, na ajira zinahitajika kwa kiasi kikubwa kwa
wananchi hususani vijana ambao ndio nguvu kazi ya Taifa” Amesisitiza Prof
Mkenda
Kadhalika amewashukuru wadau
wote ikiwemo Benki ya NMB ili kuwezesha upatikanaji wa fedha katika hatua hii
ya awali katika kuimarisha miundombi ya kilimo hicho.
Waziri Mkenda amesema kuwa
vijana wengi wanaweza kubadilisha mtazamo ikiwa ni pamoja na maisha yao kwa
kuingia kwenye kilimo kwani serikali inaendelea kuweka miundombinu rafiki
katika sekta ya kilimo.
“Kilimo kinalipa lakini
endapo mkulima atakubaliana na mkakati wa kuongeza tija na uzalishaji sasa
Kilimo cha Pilipili tayari kina soko na fursa bado ni kubwa kwa vijana kuwekeza
kwa wingi” Amekaririwa Prof Mkenda
Waziri wa Kilimo Prof Adolf
Mkenda amewaomba wananchi wilayani Mvomero kujitolea mashamba yao ili vijana
wengi waweze kujiajiri katika sekta ya kilimo.
Mkuu wa Wilaya ya Mvomero Mhe Halim Okash amesema kuwa mradi huo wa kuendeleza sekta ya kilimo umekuja kwa wakati muafaka kwani suala la ajira kwa vijana limekuwa tatizo kubwa.
0 Comments