Viongozi wa Wizara ya Fedha na Mipango,Nishati pamoja na TANESCO wakimsikiliza Mratibu wa Mradi wa kituo cha kupoza umeme Zuzu, Mhandisi Peter Kigadye walipotembelea na kukagua ujenzi wa kituo cha kupoza umeme cha Zuzu leo Julai 26,2021 kilichopo jijini Dodoma.
Viongozi wa Wizara ya Fedha na Mipango,Nishati pamoja na TANESCO wakimsikiliza Mhandisi wa Kituo cha Zuzu Nzingula Sospeter walipotembelea na kukagua ujenzi wa kituo cha kupoza umeme cha Zuzu leo Julai 26,2021 kilichopo jijini Dodoma.
Baadhi ya Mitambo inayofanya kazi katika kituo cha kupoza umeme cha Zuzu kilichopo jijini Dodoma.
Viongozi wa Wizara ya Fedha na Mipango,Nishati pamoja na TANESCO wakiendelea na ziara ya kutembelea na kukagua ujenzi wa kituo cha kupoza umeme cha Zuzu leo Julai 26,2021 kilichopo jijini Dodoma.
...................................................................................
Na Alex Sonna,Dodoma
Viongozi wa Wizara ya Fedha na Mipango,Nishati pamoja na TANESCO wameridhishwa na utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa njia kuu ya kusafirisha Umeme (Backbone) awamu ya pili kituo cha Zuzu Jijini Dodoma.
Akizungumza leo Julai 26,2021,wakati wa ziara ya kukagua kituo hicho cha kupooza umeme kilichopo Zuzu Jijini Dodoma, Kamishna wa Fedha za Nje kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Sauda Msemo ambaye alimwakilisha Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo amesema wameridhishwa na jinsi ambavyo mradi huo unatekelezwa.
“ Sisi tumeridhishwa na utekelezaji ikiwa na mikakati mbalimbali ambayo imefikiwa ya kuhakikisha miradi inafikiwa, tunaendelea kushirikiana vizuri sisi Wizara ya Fedha na Mipango na wenzatu wa Wizara ya Nishati na Tanesco ili kuhakikisha tunafikia malengo kwa mafanikio makubwa,” amesema
Amesema wamefika katika kituo hicho ili kuona hatua iliyofikiwa katika utekelezaji wa mradi na kuwa na uwezo wa kupokea umeme wa kiwango kinachotakiwa
“Huu ni mwendelezo wa ziara tulianzia katika Bwawa la Mwalimu Nyerere tukafuatiwa na Kinyerezi kisha Chalinze kuona zile substation (vituo vya umeme) kwa hiyo nimwendelezo ilikuwa na lengo la kuona miradi hii na hatua ambazo zimechukuliwa,”amesema.
Amesema Wizara ya Fedha na Mipango itaendelea kutoa fedha kwa ajili ya miradi mbalimbali ambayo ina manufaa kwa nchi huku ikiendelea kusisitiza umuhimu wa ushirikiano ili kutekeleza miraji yenye tija.
“ Tumekuwa tukitoa fedha vizuri na kwa wakati sisi tunaendelea kushirkiana kwa karibu kwa sababu tunaelewa umuhimu wa miradi hii kwa hiyo Wizara ya Fedha na Mipango inaendelea kusisitizia suala la ushirikiano na chochote kinachotokea ili kuwe na uelewa wa pamoja,”amesema.
Kwa upande wake, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Kheri Mahimbali amesema wamekamilisha ziara ya kukagua kituo hicho cha kufufua umeme na wamefarijika kwa viongozi hao kufika katika kituo hicho.
“ Tumekamilisha ile ziara ambayo tumeanza nayo ambapo wameangalia tutakavyoutoa umeme kutoka Julius Nyerere mpaka chalinze na kutoka Chalinze mpaka Dodona, kwa ujumla sisi tumefarijika kuwapata viongozi kuja kutembelea ni wadau muhimu kwetu.
“ Tumepata fursa ya kuweza kujadiliana na kuwa na uelewa wa pamoja na tunatumai baada ya ziara hii itasaidia zaidi katika majukumu yao katika sekta ya nishati,”amesema.
Kwa upande wake, Mhandisi Mkuu kutoka Shirika la Umeme Tanzania Dodoma, Donasiano Shamba amesema wamenufaika na mradi huo kwani Megawati zimeweza kuongezeka.
“Sisi kama watumiaji Mkoa wa Dodoma tumenufaika sana na mradi huu huko nyuma tulikuwa na Megawati 34 ina maana transfoma zilizokuwepo zilikuwa ni mbili ambazo Capacity yake ilikuwa jumla ni Megawati 32 lakini baada ya mradi huu ambao umeongeza transfoma 2 kila moja ilikuwa na uwezo megawati 100 hivyo tumekuwa na megawati 200,”amesema.
Amesema miaka ya nyuma umeme wa Mkoa wa Dodoma haukuwa katika hali nzuri lakini baada ya kuongeza transfoma umeme umekuwa vizuri.
“ Mwaka 2015 tulikuwa na wateja wachache lakini baada ya Serikali kuhamia Dodoma wananchi wameongezeka sana sasa hivi tuna wateja zaidi ya 160,000 kwahiyo hiyo yote sababu ya uwepo wa kituo hiki inatupa uwezo wa kuendela kuwahudumia wananchi,”amesema.
Naye Mratibu wa Mradi wa kituo cha kupoza umeme Zuzu, Mhandisi Peter Kigadye, amesema kuwa ujenzi wa njia kuu ya kusafirisha Umeme (Backbone) awamu ya pili, gharama za mradi huo ni Dola milioni 54.3 pamoja na kituo cha Mkoani Singida.
Mhadisi Kigadye amesema mradi kama huo unatakelezwa katika vituo vinne vya Iringa, Shinyanga, Singida, Iringa na Dodoma.
Akikizungumzia kituo cha Zuzu, kigadye amesema ni muhimu kwani kitapokea umeme kutoka katika Bwawa la Mwalimu Julius Nyerere na kupeleka maeneo ya Kaskazini mwa Nchi kupitia Singida na maeneo ya Kusini kupitia Iringa.
Amesema kituo hichi kinatarajia kukamilika Septemba mwaka huu huku akidai changamoto waliyokutana nayo ni katika uingizaji wa vifaa kutokana na kuzuiliwa kwa safari kwa sababu ya janga la ugonjwa wa Corona.
0 Comments