Mamlaka ya Elimu Nchini(TEA) imetunukiwa cheti cha utambuzi kutokana na mchango wake katika kuboresha mioundombinu ya elimu nchini kupitia Mfuko wa Elimu wa Taifa ambao TEA inausimamia.
Cheti Cheti hicho kimetolewa na Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga kutokana na TEA kufadhili ujenzi wa madarasa, nyumba za walimu na mabweni katika Halmashauri hiyo ambapo Zaidi ya Shilingi Milioni 300 zimetumika katika miradi hiyo .
Mbunge wa Jimbo la Kwela, Mhe. Deus Clement Sangu amekabidhi cheti hicho kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania, Bi. Bahati Geuzye na kushuhudiwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga, Mhe. Kalolo Gerald Ntilla na Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga Wilfred A. Lazaro na wajumbe wa Menejimenti ya TEA.
Akizungumza katika hafla hiyo fupi, Mbunge wa Kwela, Mhe. Sangu, amesema Mamlaka ya Elimu Tanzania inafanya kazi nzuri ya kuboresha miundombinu ya elimu katika jimbo lake na maeneo mengine ya nchi, hali ambayo inaakisi utekelezaji mzuri wa Ilani ya chama tawala ambayo pamoja na mambo mengine imelenga kuboresha miundombinu ya elimu nchini. “Utekelezaji makini wa miradi ya TEA, unaonyesha ni kwa namna gani Mamlaka inatekeleza kwa vitendo utekeleza ilani ya Serikali iliyopo madarakani” Amesema Mhe. Sangu
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa TEA, Bi Bahati Geuzye ametumia fursa hiyo kuwataka wadau kuitunza vyema miradi inayofadhiliwa kupitia Mfuko wa Elimu wa Taifa ili inufaishe watanzania wengi. Amekumbusha matumizi sahihi ya fedha zinazotolewa kufadhili miradi hiyo ili ijengwe katika ubora unaokusudiwa.
TEA) ni Taasisi ya Umma iliyoanzishwa chini ya kifungu cha (5)1 cha Sheria ya Mfuko wa Elimu Namba 8 ya Mwaka 2001, ili kusimamia Mfuko wa Elimu wa Taifa ulioanzishwa chini ya Sheria hiyo. TEA inatekeleza majukumu yake chini ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia.
Mbunge wa Jimbo la Kwela, Mhe. Deus Clement Sangu (wa pili kulia) akimkabidhi Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania, Bi. Bahati Geuzye ( wa pili kushoto) cheti cha pongezi na utambuzi wa mchango wa TEA katika kuboresha miundombinu ya elimu
Mbunge wa Jimbo la Kwela, Mhe Deus Clement Sangu akisistiza jambo baada ya Kukabidhi Cheti cha Kutambua Mchango wa TEA Katika Kuboresha Miundombinu ya Elimu Katika Halmashauri hiyo
Ujumbe wa Watendaji wa Kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga ukiongozwa na Mbunge wa Jimbo la Kwela, Mhe Deus Clement Sangu ukiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Menejimenti wa TEA Baada ya Kukabidhi Cheti cha Kutambua Mchango wa TEA Katika Kuboresha Miundombinu ya Elimu Katika Halmashauri hiyo
Cheti ambacho Mamlaka ya Elimu Nchini(TEA) imetunukiwa Kwa kutambua Mchango wa elimu Katika Kuboresha Miundombinu ya Elimu Katika Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga.
0 Comments