Kwa mara nyingine klabu ya Simba Sc imefanikiwa kulinyakuwa taji la kombe la Shirikisho la Azam Sport federation Cup (ASFC) mara baada ya kuwafunga mahasimu wao Yanga kwa bao 1-0 kwenye mchezo huo ambao ulipigwa katika dimba la Tanganyika Mkoani Kigoma.
Ni kiungo wa kimataifa wa Kenya Tadeo Lwanga alihamsha hisia za mashabiki wa msimbazi mara baada ya kuutendea haki kona iliyopigwa na beki Mohammed Hussein na kuweza kupachika bao kwa kichwa dakika ya 79 ya mchezo.
Yanga ilicheza pungufu kipindi cha pili mara baada ya kiungo wao wa kimataifa wa Congo DR Mukoko Tonombe kupewa kadi nyekundu mara baada ya kumchezea rafu John Bocco kwa kumpiga kiwiko kwa nyuma.
0 Comments