Katibu wa NEC ya CCM, Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka |
Kimesema muktadha na msingi wa maneno ya Mbatia yanaweza kutafsirika yamekusudia kuwachochea wananchi na kuwagombanisha na serikali halali iliyowekwa kidemokrasia, kisheria na kikatiba.
Matamshi hayo yametamkwa jana na katibu wa itikadi na uenezi shaka Hamdu Shaka katika ofisi ndogo za CCM lumumba ambae alisema matamshi ya Mbatia yamekosa simile na nidhamu kwani yamedhamiria kupandikizia chuki wananchi jambo ambalo halikubaliki na zaidi yamejaa uongo na upotoshaji.
Shaka alisema ahadi ya Rais Samia kusema suala la katiba liwekwe kando kwa muda ili ajenge uchumi wa taifa mantiki yake si kubeza au kupuuza usiwepo mchakato wa kupatikana katiba mpya ambayo ipo hatua ya katiba inayopendekezwa bali kila jambo ni muhimu kupanga lipi lianze na lipi lifuate.
Alisema hata Mbatia na wenzake katika miaka ya mwishoni mwa 1990 walidai usiruhusiwe mfumo wa vyama vingi kabla ya kuitishwa mkutano wa kitaifa wa katiba badala yake bunge la chama kimoja likaitunga sheria namba 5 ya mwaka 1992 ilioruhusu demokrasia ya vyama vingi na mambo yakaendelea.
"Serikali bila shinikizo la ndani na nje iliunda tume ya jaji Francis Nyalali na kuanza kwa mchakato wa ukusanyaji wa maoni ya wananchi. Mwaka 1992 bunge la chama kimoja bila kuwepo upinzani likatunga sheria Namba 5 ya mwaka 1992 na mbatia akabahatika kuwa mbunge mwaka 1995" Alisema
Alimtaka mwenyekiti huyo wa NCCR-MAGEUZI kuacha kutamka maneno ambayo yamelenga kuamsha shari na hasama kwani yeye na wenzake waelewe hawana namna ya kuilazimisha serikali ifanye watakavyo kwa matakwa yao.
"Mbatia na wenzake walilikimbia bunge maalum la katiba ambalo lilikuwa na jukumu la kutunga katiba mpya. Sababu ikiwa ni kushindwa kuheshimu demokrasia inayotegemea ujenzi wa hoja na kuheshimu kutofautiana mtazamo na mawazo. Hivyo hawana dhamira wala nia ya kuipata katiba mpya bali wanataka kuutumia mchakato huo kama fursa ya kuhamasisha vurugu nchini jambo ambalo kamwe halitapewa nafasi na Serikali za CCM" Alisema shaka
Amefahamisha kuwa ajenda ya katiba mpya ilikuwa ni ajenda CCM tokea mwaka 2005 hatimaye mchakato wake ukaanzishwa na Rais wa awamu ya nne Mheshimiwa Dkt Jakaya Kikwete mpaka kupatikana kwa katiba inayopendekezwa inayosubiri kupigiwa kura ya maoni pale serikali itakapoona ni muda na wakati muafaka kufanya hivyo. Hawa wanaojipa kazi ya kuidai katiba mpya leo ndio waliokimbia na kususia fursa ya kushiriki zoezi hilo wakati lilipokuwa likifanyika. Mashinikizo yenye malengo hasi hayana nafasi Tanzania.
"Serikali ya Tanzania inao uzoefu wa kufanya mambo yake yenyewe bila kushurutishwa. Hii ndio sababu Tanzania imeendelea kuwa Taifa la amani. Uamuzi wa kuridhia mchakato wa katiba mpya kipindi cha mwaka 2012-2014 ni uthibitisho wa hilo"
Alieleza kuwa hata kudorora na kusuasua kwa NCCR-MAGEUZI na vyama vingine kukimbiwa na baadhi ya wanachama na viongozi wake tatizo si kukosekana kwa katiba mpya bali usultani na udikteta ndani ya vyama hivyo unaokataa mabadiliko ya fikra hivyo kuona wawaachie vyama vyao vilivyogeuzwa kampuni binafsi.
"Ifike pahala kila mtu lazima aielewe hadhi na heshima ya Rais.Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimesema matamshi ya Mwenyekiti wa NCCR-MAGEUZI James Francis Mbatia aliyedai Rais Samia Saluhu Hassan kuwapa muda wanasiasa ili azungumze nao likiwemo suala la katiba mpya na kudai bila kufanya hivyo ni kuliparaganya Taifa ni matamshi ya kichochezi.
Kimesema muktadha na msingi wa maneno ya Mbatia yanaweza kutafsirika yamekusudia kuwachochea wananchi na kuwagombanisha na serikali halali iliyowekwa kidemokrasia, kisheria na kikatiba.
Matamshi hayo yametamkwa jana na katibu wa itikadi na uenezi shaka Hamdu Shaka katika ofisi ndogo za CCM lumumba ambae alisema matamshi ya Mbatia yamekosa simile na nidhamu kwani yamedhamiria kupandikizia chuki wananchi jambo ambalo halikubaliki na zaidi yamejaa uongo na upotoshaji.
Shaka alisema ahadi ya Rais Samia kusema suala la katiba liwekwe kando kwa muda ili ajenge uchumi wa taifa mantiki yake si kubeza au kupuuza usiwepo mchakato wa kupatikana katiba mpya ambayo ipo hatua ya katiba inayopendekezwa bali kila jambo ni muhimu kupanga lipi lianze na lipi lifuate.
Alisema hata Mbatia na wenzake katika miaka ya mwishoni mwa 1990 walidai usiruhusiwe mfumo wa vyama vingi kabla ya kuitishwa mkutano wa kitaifa wa katiba badala yake bunge la chama kimoja likaitunga sheria namba 5 ya mwaka 1992 ilioruhusu demokrasia ya vyama vingi na mambo yakaendelea.
"Serikali bila shinikizo la ndani na nje iliunda tume ya jaji Francis Nyalali na kuanza kwa mchakato wa ukusanyaji wa maoni ya wananchi. Mwaka 1992 bunge la chama kimoja bila kuwepo upinzani likatunga sheria Namba 5 ya mwaka 1992 na mbatia akabahatika kuwa mbunge mwaka 1995" Alisema
Alimtaka mwenyekiti huyo wa NCCR-MAGEUZI kuacha kutamka maneno ambayo yamelenga kuamsha shari na hasama kwani yeye na wenzake waelewe hawana namna ya kuilazimisha serikali ifanye watakavyo kwa matakwa yao.
"Mbatia na wenzake walilikimbia bunge maalum la katiba ambalo lilikuwa na jukumu la kutunga katiba mpya.
Sababu ikiwa ni kushindwa kuheshimu demokrasia inayotegemea ujenzi wa hoja na kuheshimu kutofautiana mtazamo na mawazo.
Hivyo hawana dhamira wala nia ya kuipata katiba mpya bali wanataka kuutumia mchakato huo kama fursa ya kuhamasisha vurugu nchini jambo ambalo kamwe halitapewa nafasi na Serikali za CCM" Alisema shaka
Amefahamisha kuwa ajenda ya katiba mpya ilikuwa ni ajenda CCM tokea mwaka 2005 hatimaye mchakato wake ukaanzishwa na Rais wa awamu ya nne Mheshimiwa Dkt Jakaya Kikwete mpaka kupatikana kwa katiba inayopendekezwa inayosubiri kupigiwa kura ya maoni pale serikali itakapoona ni muda na wakati muafaka kufanya hivyo.
Hawa wanaojipa kazi ya kuidai katiba mpya leo ndio waliokimbia na kususia fursa ya kushiriki zoezi hilo wakati lilipokuwa likifanyika. Mashinikizo yenye malengo hasi hayana nafasi Tanzania.
"Serikali ya Tanzania inao uzoefu wa kufanya mambo yake yenyewe bila kushurutishwa. Hii ndio sababu Tanzania imeendelea kuwa Taifa la amani. Uamuzi wa kuridhia mchakato wa katiba mpya kipindi cha mwaka 2012-2014 ni uthibitisho wa hilo"
Alieleza kuwa hata kudorora na kusuasua kwa NCCR-MAGEUZI na vyama vingine kukimbiwa na baadhi ya wanachama na viongozi wake tatizo si kukosekana kwa katiba mpya bali usultani na udikteta ndani ya vyama hivyo unaokataa mabadiliko ya fikra hivyo kuona wawaachie vyama vyao vilivyoanza kampuni binafsi.
"Ifike pahala kila mtu lazima aielewe hadhi na heshima ya Rais. Anaposema kiongozi wa dola ataiparaganya nchi ni maneno yakizandiki.
Hata Mabatia anaposema vurugu zinazoendelea Afrika kusini zitatokea Tanzania bila shaka anatamani ghasia za aina hiyo kutokea hapa.
Mwanasiasa wa aina hii ni hatari kwa amani, umoja na utulivu wa nchi yetu wananchi wampuuze. Watu wafahamu ulimi ni kinyama kidogo hatari usipotumika vizuri"Alisisitiza shaka
Aidha Shaka alisema kwa bahati mbaya sana imejengeka dhana kuwa demokrasia ni pale tu upinzani unapofanikiwa au chama tawala kinaposhindwa, amesisitiza dhana hiyo si sawa na wakati umefika kwa upinzani kubadilika kwani watanzania wamekuwa na mwamko wa mambo wasitegemee kuwa wataendelea kuwaburuza kama ilivyokuwa miaka ya nyuma. Anaposema kiongozi wa dola ataiparaganya nchi ni maneno yakizandiki. Hata Mabatia anaposema vurugu zinazoendelea Afrika kusini zitatokea Tanzania bila shaka anatamani ghasia za aina hiyo kutokea hapa.
Mwanasiasa wa aina hii ni hatari kwa amani, umoja na utulivu wa nchi yetu wananchi wampuuze. Watu wafahamu ulimi ni kinyama kidogo hatari usipotumika vizuri"Alisisitiza shaka
Aidha Shaka alisema kwa bahati mbaya sana imejengeka dhana kuwa demokrasia ni pale tu upinzani unapofanikiwa au chama tawala kinaposhindwa, amesisitiza dhana hiyo si sawa na wakati umefika kwa upinzani kubadilika kwani watanzania wamekuwa na mwamko wa mambo wasitegemee kuwa wataendelea kuwaburuza kama ilivyokuwa miaka ya nyuma.
0 Comments