Ticker

6/recent/ticker-posts

SEMINA YA WASTAAFUU WATARAJIWA PSSSF YAFANYIKA MWANZA

 *RC: Wekezeni katika miradi rafiki

*Msikurupuke kuanzisha miradi, jifunzeni kwanza

*Aipongeza PSSSF kwa semina

Na Mwandishi Wetu, Mwanza

MKUU wa Mkoa wa Mwanza, Mhe. Mhandisi Robert Gabriel amewashauri Wastaafu watarajiwa wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) kuwekeza katika miradi waliyoizoea ili waweze kuindesha vyema na kwa faida.

Mhandisi Gabriel alisema hayo Jijini Mwanza wakati wa ufunguzi wa Semina ya Wastaafu watarajiwa kwa wanachama wa PSSSF wa mkoa wa mwanza inayofanyika Julai 26 hadi 27, 2021.

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Mhandisi Robert Gabriel, akihutubia wakati akifungua semina ya Wastaafu watarajiwa wa PSSSF. Kulia ni Mwakilishi wa Mkurugenzi wa PSSSF, Bi. Beatrice Musa-Lupi na katika ni Bi. Nyamisinda Manyunyi kutoka NMB.

“Kama unataka kuingia katika mradi wowote, hakikisha unaonana na wataalamu ili waweze kukusaida katika uwekeza sahihi na wenye tija,” alisauri Bw. Gabriel

Aliwashauri wastaafu hao watarajiwa watakapolipwa mafao yao wasikurupuke kuanzisha miradi bali yajifunze vyema mradi wanaotaka kuwekeza ili wajue njia sahihi ya kuwekeza katika mradi huo

“PSSSF wameletea Mabenki na Taasisi mbalimbali ili muweze kupata uelewa na maarif ili mfanye maamuzi sahihi ya uwekezaji. Hivyo tumieni fursa vyema, hii bahati kubwa kwenu, kwani sio wote wanaopata fursa kama hii,” alisema Mkuu wa mkoa wa Mwanza.

Post a Comment

0 Comments