Rais wa Chama Cha Wachimbaji wa Madini Tanzania (FEMATA), John Bina akizungumza leo Julai 27,2021 wakati akitembelea mabanda ya washiriki wa Maonesho ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga yanayofanyika katika uwanja wa Zainab Telack kijiji cha Butulwa kata ya Old Shinyanga Manispaa ya Shinyanga.
Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Rais wa Chama Cha Wachimbaji wa Madini Tanzania (FEMATA), John Bina amelaani vitendo vya Utoroshaji madini na kuwaonya baadhi ya wachimbaji wa madini wanaotorosha madini na baadhi ya watu wanaoshiriki utoroshaji madini.
Rais huyo wa FEMATA ameyasema hayo leo Jumanne Julai 27, wakati akitembelea mabanda mbalimbali ya washiriki wa Maonesho ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga yanayofanyika katika uwanja wa Zainab Telack kijiji cha Butulwa kata ya Old Shinyanga Manispaa ya Shinyanga.
"Shinyanga na Chunya bado yana utoroshaji wa madini. Natumia nafasi hii kulaani utoroshaji wa madini. Nawaonya wachimbaji madini na baadhi ya watu wanaoshiriki utoroshaji madini kuacha mara moja tabia hiyo",amesema Bina.
Bina amesema Wachimbaji Wadogo wengi wao hawana mitaji ya kununua Miundo Michundo ‘Pembejeo za uchimbaji’ hivyo kuziomba Taasisi za Kifedha kuangalia njia nzuri ya kuwasaidia Wachimbaji Wadogo wa Madini kwa kuwapatia mikopo kwani hivi sasa bado kuna ugumu katika kuwakopesha wachimbaji hao.
Pia Rais huyo wa FEMATA amesema Viongozi wa Vyama vya Wachimbaji Madini ni lazima wawe wanajishughulisha na uchimbaji madini badala ya kuwa na viongozi wasio wachimbaji ili kupunguza migogoro kwa wachimbaji madini.
Afisa Madini Mkazi Mkoa wa Shinyanga, Mhandisi Joseph Kumbulu amesema milango ya kutoa leseni kwa wanaotaka kufanya shughuli za uchimbaji iko wazi hivyo wafike katika ofisi kwake kwa ajili ya kupewa utaratibu huku akibainisha kuwa Suala la Madini halibagui mtu yeyote hivyo kila mtu anaruhusiwa kuchimba madini.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Wachimbaji Madini mkoa wa Shinyanga ‘Shinyanga Region Miners Association – SHIREMA', Hamza Tandiko na Mkurugenzi wa Kampuni ya ShyGem Limited ambaye ni Katibu Mkuu wa SHIREMA na Mhazini Mkuu wa FEMATA, Gregory Kibusi wameomba Makampuni ya Wachimbaji Wazawa yapewe Ruzuku au Mikopo nafuu ili wanunue vifaa vya kisasa vya kuchimbia ili waweze kuwa na uzalishaji mkubwa wa madini na wenye tija.
Naye Mkurugenzi wa Kampuni ya Uundaji wa Vifaa vya Uchimbaji na Uchenjuaji Madini ya Shinyanga Best Iron, Kashi Salula ameziomba Taasisi za Fedha zikiwemo Benki ziwakopeshe Wachimbaji Wadogo wa Madini ili wanunue Miundo Michundo ‘Pembejeo za uchimbaji’ kutokana na wengi wao kutokuwa na mitaji ya kununua mitambo hiyo ya kuchimba na kuchenjua madini huku akiomba maeneo ya machimbo yafungiwe Transfoma ili kupata huduma ya umeme kwa ajili ya kupunguza gharama za uchimbaji.
"Tunaishukuru Serikali kwa kupeleka umeme vijijini lakini umeme huu ni kwa ajili ya majumbani tu, sisi Wachimbaji wadogo wa madini changamoto yetu ni umeme, umeme uliopo haujatunufaisha tunaomba Serikali ifunge Transfoma kwenye maeneo ya machimbo ili tupate umeme wenye nguvu",amesema Kashi.
ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Rais wa Chama Cha Wachimbaji wa Madini Tanzania (FEMATA), John Bina akizungumza leo Julai 27,2021 wakati akitembelea mabanda ya washiriki wa Maonesho ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga yanayofanyika katika uwanja wa Zainab Telack kijiji cha Butulwa kata ya Old Shinyanga Manispaa ya Shinyanga.Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mwenyekiti wa Chama cha Wachimbaji Madini mkoa wa Shinyanga ‘Shinyanga Region Miners Association – SHIREMA, Hamza Tandiko akizungumza kwenye Maonesho ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga yanayofanyika katika uwanja wa Zainab Telack kijiji cha Butulwa kata ya Old Shinyanga Manispaa ya Shinyanga.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Uundaji wa Vifaa vya Uchimbaji na Uchenjuaji Madini ya Shinyanga Best Iron, Kashi Salula akimweleza Rais wa Chama Cha Wachimbaji wa Madini Tanzania (FEMATA), John Bina changamoto wanazokutana nazo wachimbaji wadogo wa madini ambapo ameziomba Taasisi za Fedha zikiwemo Benki ziwakopeshe Wachimbaji Wadogo wa Madini ili wanunue Miundo Michundo ‘Pembejeo za uchimbaji’ kutokana na wengi wao kutokuwa na mitaji ya kununua mitambo hiyo ya kuchimba na kuchenjua madini.
Rais wa Chama Cha Wachimbaji wa Madini Tanzania (FEMATA), John Bina akizungumza kwenye banda la Shinyanga Best Iron. Kulia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Uundaji wa Vifaa vya Uchimbaji na Uchenjuaji Madini ya Shinyanga Best Iron, Kashi Salula.
Rais wa Chama Cha Wachimbaji wa Madini Tanzania (FEMATA), John Bina akizungumza kwenye banda la Shinyanga Best Iron. Kulia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Uundaji wa Vifaa vya Uchimbaji na Uchenjuaji Madini ya Shinyanga Best Iron, Kashi Salula.
Afisa Madini Mkazi Mkoa wa Shinyanga, Mhandisi Joseph Kumbulu akizungumza kwenye kwenye banda la Shinyanga Best Iron kwenye Maonesho ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga.
Mkurugenzi wa Kampuni ya ShyGem Limited ambaye ni Katibu Mkuu wa Chama cha Wachimbaji Madini mkoa wa Shinyanga ‘Shinyanga Region Miners Association – SHIREMA na Mhazini Mkuu FEMATA, Gregory Kibusi akionesha Mtambo wa kuosha na kutenganisha mchanga wa madini ya Almasi (Diamond Srabber) wakati Rais wa Chama Cha Wachimbaji wa Madini Tanzania (FEMATA), John Bina akitembelea banda la ShyGem Ltd kwenye Maonesho ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga.
Mkurugenzi wa Kampuni ya ShyGem Limited ambaye ni Katibu Mkuu wa Chama cha Wachimbaji Madini mkoa wa Shinyanga ‘Shinyanga Region Miners Association – SHIREMA na Mhazini Mkuu FEMATA, Gregory Kibusi akielezea namna shughuli ya kuchenjua madini ya Almasi wakati Rais wa Chama Cha Wachimbaji wa Madini Tanzania (FEMATA), John Bina akitembelea banda la ShyGem Ltd kwenye Maonesho ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga.
Afisa Madini Mkazi Mkoa wa Shinyanga, Mhandisi Joseph Kumbulu akionesha Madini ya Almasi banda la ShyGem Ltd kwenye Maonesho ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
0 Comments