Ticker

6/recent/ticker-posts

NEMC WASHIRIKIANA NA SUA KUZINDUA WARSHA YA MRADI WA UTAFITI WILAYANI MBARALI MKOANI MBEYA

Mkuu wa Wiyala ya Mbalali Reuben Mfune

WADAU nchini wametakiwa kuhakikisha  wanalinda rasilimali maji kikamilifu kwa ajili ya uendelevu wa madakio ya maji na maisha kwa ujumla.   


Hayo yamesemwa leo na Mkuu wa Wilaya ya Mbarali, Reuben Mfune, wakati wa warsha ya uzinduzi wa Mradi wa utafiti wa usimamizi endelevu wa madakio ya maji kupitia tathimini ya kuimarisha mtiririko wa maji kwa mazingira na utekelezaji wake katika kulinda Ukanda wa Magharibi mwa Bahari ya Hindi kutokana na athari za shughuli za binadamu , Tanzania (EFLOWS). 

Amesema Mfune, ametoa shukrani kwa Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhifadhi wa Mazingira (UNEP) kwa ufadhili wa kifedha katika mradi huo, pia Sekretarieti ya Azimio la Nairobi (Nairobi Convection Secretariat) ambayo ni msimamizi wa utekelezaji. Pamoja na Waratibu wa mradi huo kutoka Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira (NEMC) na Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) kwa kujitoa kwao kutekeleza mradi huu ambao ni mojawapo ya miradi iliyopo katika nchi zilizo kwenye Mpango Mkakati wa nchi za Magharibi mwa Ukanda wa Bahari ya Hindi. 
 
Aidha, amesema kuwa anafurahi kuona kwamba masuala ya mazingira kama vile umwagiliaji, kilimo kandokando ya kingo za mito, ufugaji wa mifugo ndani ya kidakio cha mto Mbarali na Bonde la Rufiji pamoja na ongezeko la watu, vinasimamiwa kwa uhifadhi kamilifu wa eneo la Magharibi mwa Ukanda wa Bahari ya Hindi. Na muhimu zaidi kwa ajili ya mtiririko endelevu wa maji kuelekea Mradi wa kufua umeme wa Mwalimu Nyerere (Julius Nyerere Hydro Power Project - JNHPP).

Naye Mkurugenzi Mkuu wa NEMC katika hotuba yake ya ukaribisho kwa mgeni Rasmi iliyosomwa kwa niaba yake na Meneja wa Utafiti-NEMC Bi Rose Salema Mtui amesema kuwa NEMC kwa kushirikiana na taasisi za kitaaluma/utafiti zimekuwa zikitengeneza miradi/programu na kufanya tafiti na mojawapo ni kama mradi huo uliozinduliwa kwa lengo la kutatua matatizo mbalimbali ya kimazingira. 
Meneja Tafiti za Mazingira Baraza la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), Rose Mtui

“Kupitia mradi huu, utekelezaji wa mtiririko wa maji kwa mazingira (env. flow) ni muhimu sana kwa uendelevu wa ikolojia ya mto; na natumaini wadau wote na Serikali kwa ujumla watakuwa tayari kutoa ushirikiano mkubwa kuhakikisha malengo ya mradi huu yametimia” alisema.

Akiongea katika warsha hiyo ya Uzinduzi Mkurugenzi wa Shahada za Juu Uhawilishwaji wa teknolojia za Kitafiti kutoka Chuo Cha Sokoine SUA Profesa Ezron Karimuribo amesema kuwa kuna uharibifu mkubwa wa vyanzo vya maji Nchini na umetokana na shughuli mbalimbali za kibinadamu kama vile ukataji miti, uchomaji misitu, kilimo pembezoni mwa vyanzo vya maji, uchimbaji madini,ufuagji na uchepushaji wa maji. Hivyo basi katika mradi huo ambao utafanyika katika wilaya ya Mbarali na wilaya hiyo imechukuliwa kama kianzio tu.

Mradi huo utafiti wa usimamizi endelevu wa madakio ya maji kupitia tathimini ya kuimarisha mtiririko wa maji kwa mazingira na utekelezaji wake katika kulinda Ukanda wa Magharibi mwa Bahari ya Hindi kutokana na athari za shughuli za kibinadamu, Tanzani(EFLOWS unaratibiwa na Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) na Chuo cha Kilimo cha Sokoine (SUA).

Post a Comment

0 Comments