Makamu wa Rais amesema Serikali inaendelea na ujenzi wa Hospitali, zahanati na vituo vya afya katika mkoa wa Mtwara ili kuwasogezea huduma za afya wananchi ikiwa ni pamoja na kuhakikisha upatikanaji wa madawa, vifaa tiba na vitendanishi.
Aidha amesema serikali itaendelea kuajiri watumishi wa sekta ya afya na sekta nyingine na kuutaka uongozi wa Mkoa wa Mtwara kuimarisha utaratibu wa utoaji dawa na kuhakikisha hakuna upotevu wa dawa. Amesema Serikali itachukua hatua kali kwa yeyote atakayefanya uzembe au kuhusika na wizi wa dawa hizo ikiwemo kutaifishwa kwa mali za yeyote atakayehusika katika wizi huo.
Makamu wa Rais ametoa wito kwa taasisi za serikali zinazotekeleza ujenzi wa miradi mbalimbali kuendelea kuwatumia Shirika la Nyumba la Taifa pamoja na malighafi zinazokidhi viwango kutoka nchini Tanzania kama ilivyofanyika katika ujenzi wa Hospitali hiyo.
Akiwa Hospitalini hapo Makamu wa Rais amewapongeza wananchi wa Mtwara kwa juhudi zao za kutunza mazingira ambao kuanzia mwaka 2021 uanze, wamepanda miti ya kawaida 4,480,600 kati ya hiyo, miti 4,312,74,3 imestawi.
Kwa upande wake Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Godwin Mollel amesema tayari Wizara ya Afya imepata kibali cha kuajiri watumishi mia tatu kwaajili ya Hospitali hiyo inayotarajiwa kuanza kutoa huduma mwishoni mwa mwezi Oktoba.
0 Comments