Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe, Anthony Mtaka akikabidhiwa Mwenge wa Uhuru na Mkuu wa Mkoa Singida Mhe. Bilinith Mahenge mapema hii leo Julai 25, 2021 Wilayani Bahi, Jijini Dodoma.
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana na Ajira Mhe, Patrobas Katambi (Mb) akizungumza na Viongozi wa Mkoa wa Dodoma, Singida na wakazi wa wilaya ya Bahi wakati wa mapokezi ya Mbio maalum za Mwenge wa Uhuru mkoani Dodoma.
Sehemu ya Wakazi wa Bahi wakisikiliza hotuba ya Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana na Ajira Mhe, Patrobas Katambi wakati wa makabidhiano ya Mwenge wa Uhuru Mkoa wa Singida kwenda Mkoani Dodoma.
Baadhi ya Wajumbe wa Menejimenti kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu – Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu wakifuatilia matukio mbalimbali wakati wa makabidhiano ya Mwenge wa Uhuru Mkoa wa Singida kwenda Mkoani Dodoma.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe, Anthony Mtaka akikabidhi Mwenge wa Uhuru kwa Mkuu wa Wilaya ya Bahi Mhe. Mwanahamisi Munkunda (wa pili kutoka kulia) kwa ajili ya kukimbizwa katika wilaya hiyo na ukaguzi wa miradi mbalimbali. Kulia ni Kiongozi wa Mbio maalum za Mwenge wa Uhuru LT. Josephine Mwambashi.
Kiongozi wa Mbio maalum za Mwenge wa Uhuru LT. Josephine Mwambashi (kulia) akieleza jambo wakati wa makabidhiano ya Mwenge wa Uhuru Mkoa wa Singida kwenda Mkoani Dodoma. Wa pili kutoka kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe, Anthony Mtaka.
PICHA NA OFISI YA WAZIRI MKUU
(SERA, URATIBU, BUNGE, KAZI, VIJANA, AJIRA NA WENYE ULEMAVU)
0 Comments