Ticker

6/recent/ticker-posts

JIKO LA MKAA LAUA WAPENZI MKOANI NJOMBE

**************************

NJOMBE Watu wawili wanaodaiwa kuwa ni wapenzi wamefariki dunia mkoani Njombe baada ya kuweka jiko la mkaa katika chumba walichokuwa wanalala ili kupunguza ukali wa baridi.


Akizungumza na vyombo vya habari kamanda wa jeshi la polisi mkoani Njombe Hamis Issa amesema watu hao waliofahamika kwa jina la Benitho Mbata  ambaye ni mkazi wa national Housing mjini Njombe na Jazira Said Mkazi wa Namtumbo wamefariki dunia kutokana na gesi hatari ya mkaa na kuwataka wananchi kutafuta njia za kukabiliana na baridi ikiwemo kuvaa mavazi mazito badala ya kukoleza mkaa na kisha kuweka jiko vyumbani. 


  Katika hatua nyingine kamanda Issa amesema kuna tukio jingine la kustaajabisha la mtu kufariki dunia kudondokewa na mti ambao alikuwa akiukata mwenyewe na kisha kutoa rai kwa watu wanahitaji kukata miti kuhitaji ushauri wa kitalaamu ili kunusuru maisha yao. 


  Tukio lingine ni la mtu kugongwa na bodaboda na kisha dereva kukimbia katika kijiji cha Ikonda wilayani Makete ambapo kutokana na tukio hilo kamanda Issa ametoa rai kwa madereva wote kuwa na namba za vituo ili kuthibiti matukio ya kialifu. 


  Kwa upande wake mwenye nyumba Samson Mwalongo na baadhi ya majirani wanasema kijana huyo hakuonekana kwa zaidi ya siku tatu hadi anatambulika kupoteza maisha na kudai kwamba hata mwanamke aliyepoteza maisha anadaiwa kuwa alikuwa safari kwenda Songea . 


  Katika mkoa wa Njombe kuanzia mwezi June hadi Septemba huwa ni kipindi cha baridi kali hivyo matumizi ya mkaa huongezeka.

Post a Comment

0 Comments